WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, October 14, 2013

NYERERE: WAZEE NDIO NGUZO YA NCHI


Nyerere_na_mama_yake_Bi_Mgaya_pamoja_na_mkewe_7ce1b.jpg
Na Daniel Mbega
DEMOKRASIA ya sasa imepanuka kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma, hasa kipindi cha ukoloni. Leo hii tunashuhudia hata vijana wa shule wanaifahamu vyema siasa, huku uongozi ukishikwa na vijana wadogo, wengine wakiwa hawajafikisha hata miaka 30.
Mwaka huu tunapomuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo chake, tumeona bora tuzungumze, na tulete hotuba yake, akielezea namna alivyoanza
siasa miaka ile ya 1950, mara baada ya kurejea kutoka mamsomoni Scotland.
Yeye anasema kwamba alianza akiwa 'mdogo' akiwa na miaka 30 hivi mwaka 1952 aliporejea, lakini kwa sasa ukitaja miaka hiyo huwezi amini kama hukuwakuta waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hata wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa wametopea kweli kwenye siasa.
Kwa miaka ile umri huo alikuwa bado mdogo, na hata yeye mwenyewe anakiri kwamba alikuwa kijana mdogo.
Hata hivyo, Mwalimu aliamini kwamba wazee ndio nguzo ya maendeleo ya nchi, kwani yeye mwenyewe asingeweza kufanikiwa kama si kulelewa na wazee waliompa miongozo ya kutosha hadi akafikia mahali alipofikia.
Mwalimu aliyasema haya mbele ya Baraza la Wazee wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiagana nao kabla ya kung'atuka mwaka 1985. Hebu tuungane...
"MIMI nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi. (MNYAMA)

source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment