WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 2, 2013

Wamarekani wawaambia wawakilishi wao ni “wajinga” na “wapuuzi” wanaopaswa “kupevuka”

Hasira za Wamarekeni kwa Serikali na Wawakilishi wao zimeishia kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram huku kila mmoja akilaumu upande anaoona ndiyo uliosababisha shughuli muhimu za Kiserikali kufungwa kutokana na mzozo wa bajeti baina ya Republicans wanaoshikilia Baraza la Wawakilishi, na Democrats wanaoshikiliza Seneti ya Marekani.

Maoni ya wengi yamekazia kuwafahamisha viongozi hao kuwa "hawajakomaa", ni "wajinga" na "wapuuzi" wanaopaswa
"kupevuka" ("immature", "stupid", "idiots", "grow up").

Baadhi ya wahafidhina wachache wanaojiita wawakilishi wa majimbo-mekundu (red-State) wao waliunga mkono hatua ya wawakilishi wa Republican ya kuzuia mpango wa afya wa Rais Barack Obama, hata ikiwa matokeo yake ni kusababisha baadhi ya miradi mikubwa na maarufu ya Serikali kuzorota pamoja na waajiriwa wa Serikali zaidi ya laki nane kukosa mshahara kwa kipindi kisichofahamika.

Lakini wengi wa waliotoa maoni kwenye mtandao wa Twitter walisema hawaelewi ni kwa nini viongozi wao hawakuweza kufikia muafaka ili kuinusuru Serikali.

Mmoja wao aliwaambia Wawakilishi hao kuwa hawastahili kulipwa mshahara, tena inapaswa watimuliwe kazini, "DearCongress, You should noe be getting paind. In fact, you all should be firee!" aliandika Bruce Swedal (46) mkazi wa Denver, dalali wa nyumba na viwanja ambaye anasema ana wasiwasi kuhusu mustakabali wa mauzo ya nyumba endapo mikopo inayoidhinishwa na Serikali itakauka kwa kukosa fedha za kukopesha, jambo ambalo litaathiri ajira na kipato chake.

Kufungwa kwa baadhi ya ofisi na huduma zinazotolewa na Serikali ya Marekani kumesababisha hata baadhi ya tovuti zinazohusika na huduma muhimu kama vile sensa na takwimu, kilimo na maktaba ya masuala ya kihistoria kufungwa, hata ikiwa tovuti hulipiwa ada ya usajili wa jina kwa kipindi cha mwaka mzima na 'hosting' kwa kipindi cha kati ya miezi sita na kuendelea, kwa kile kilichoelezwa kwenye tovuti hizo kuwa ni kukosekana kwa mtu atakayeweza kutoa huduma pale itakapohitajika kwa wauliza maswali au wataka ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment