WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, October 14, 2013

Simba yawa ngangari kileleni

Ramadhani Singano wa Simba akijaribu kumpita beki wa timu ya Prisons Mwangama Lugano katika mechi ya ligi kuu ya Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini jana. (Picha: na Omar Fungo)
Bao lililotokana na shuti kali kutoka mita 20 lililofungwa na kiungo Jonas Mkude, jana liliiwezesha Simba kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Bara, ilipoilaza Prisons 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 18 lakini kocha Abdallah Kibadeni aliisifu Prisons kwa kucheza vizuri na kusema timu yake, ambayo wiki ijayo itawakabili watani wa jadi Yanga kwenye uwanja huo pia, haijawa vizuri.
Mwalimu wa Prisons Jumanne Chale alisema makosa katika safu yake ya ulinzi ndiyo yaliyosababisha kupoteza mchezo huo, lakini bao la Mkude lilistahili kuwa la ushindi katika ligi yoyote duniani.
Mkude alifunga bao hilo baada ya kuuwahi nje ya eneo la hatari mpira uliokuwa umeokolewa kwa kichwa na beki ya Prisons kutokana na kona iliyopigwa na mshambuliaji Christopher Edward wa Simba.
Licha ya kuwapo kwa msitu wa wachezaji wa timu zote, shuti kali la kiungo huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars, pia lilikwenda kutinga moja kwa moja kwenye nyavu za juu kupitia karibu kabisa na kona ya kulia mwa lango la wapinzani hao.
Akiwa ametiwa hamasa na bao kali hilo, Mkude alikaribia kuipa Simba bao la pili, na kwa staili ile ile, dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho lakini shuti lake kali la mbali liliguswa kidogo na kipa wa Prisons Beno David na kuwa kona.
Prisons ambayo kwa kipigo hicho inabaki na pointi saba baada ya mechi nane, ingeweza kulinganisha idadi ya michezo na alama zake hata hivyo kama ama mshambuliaji Peter Michael angepiga shuti la nguvu zaidi ama beki Joseph Owino asingekuwa mahala muafaka wakati muafaka, mwishoni kabisa mwa mchezo.
Mpira wa juu uliodakwa na kipa Abel Dhaira katika dakika ya 89 ulionekana kuwa usingekuwa na madhara yoyote langoni mwa Simba lakini wakati akianguka ardhini, mpira uliponyoka mikononi mwa Mganda huyo na kutua kwenye mguu wa kulia wa Michael.
Shuti lake dhaifu wakati akikabwa na Gilbert Kaze liliokolewa na Owino wakati likielekea nyavuni Mganda huyo akiwa alikuwa amesimama kwenye mstari wa goli wakati wa shambulizi hilo la mwisho la mechi likifanyika.
Timu zilikuwa:
SIMBA: Abel Dhaira, Nasoro Iddi, Omar Salum (Haruna Shamte dk.38), Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abulhalim Humud, Amis Tambwe, Edward Chritopher (Zahoro Pazi dk.67), Harun Chanongo.
PRISONS: Beno David, Kimenya Mashaka, Laurian Mpalile, Nurdin Issa, Mwangama Lugano, Nimkaza Jumanne, Kwanga Julius, Jimmy Shoji, Peter Michael, Omega Seme, Jeremiah Mgunda.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment