WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 26, 2013

Chadema ' Civil War' Imepamba Moto...!

MOTOOO_3daf8.jpg
Ndugu zangu,
Chadema ' Civil War' imepamba moto. Media imeripoti kuwa leo Chadema Makao Makuu watajibu mapigo. Bado moshi wa makombora ya Zitto haujatua. Ni juzi Zitto alitoka kwenye handaki na kajibu mapigo. Na kama ilivyotarajiwa, Chadema nao wametoka kwenye handaki. Nao wamejipanga kufanya mashambulizi leo. Naam, siasa ni burudani pia. Kuna wengi watasubiri kwa hamu.(P.T)
Bila shaka, Chadema watakwenda kuyaonyesha mashimo kwenye utetezi wa Zitto juzi. Watazama sana kwenye Katiba yao na kuonyesha walivyo makini katika kuifuata.
Ni nini kinachoendelea ?
Tafsiri yangu kiini ni mgogoro wa uongozi ndani ya Chadema. Ni mgogoro wenye kuiweka Chadema kwenye hatari ya kugawanyika. Na kama nilivyobainisha juzi, unahusu uongozi na mamlaka na hususan kuelekea 2015 na mbele zaidi.
Kuna mahali wahusika, kama watataka kupata - win-win situation, itawabidi wakae meza moja na kukubaliana. Lakini, inavyoonekana sasa, hakuna mwenye haja ya matokeo ya suluhu. Ni lazima mmoja apigwe. Na kama nilivyobainisha juzi, kuwa atakayeshindwa, basi, itakuwa ni mwanzo wa mwisho wake wa kuwepo katika hali aliyo nayo sasa.
Na nilisema, kuwa ' Vita' hii itapiganwa kwanza kwenye media. Na baada ya hapo itahamia kwenye mikutano ya hadhara. Ndio, na tuisubiri ' Kamukunji' .
Maggid Mjengwa.
Iringa.

No comments:

Post a Comment