WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 26, 2013

Maalim Seif aahidi kuwaunganisha Wazanzibari

Katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama chake kitaendelea na dhamira ya kuwaunganisha wananchi ili kuhakikisha kuwa Wazanzibari wanakuwa kitu kimoja katika kudai mamlaka ya Zanzibar.
Hamad alitoa msimamo huo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama chake na kusema iwapo Wazanzibari wataondosha tofauti zao na kusimamia maslahi ya nchi, maendeleo makubwa yanaweza kupatikana ikiwa ni pamoja na kuwakomboa vijana kutokana na ukosefu wa ajira.

Mkutano huo uliyofanyika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi Unguja na Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alikuwa akihitimisha ziara yake ya kichama kwa majimbo tisa ya wilaya hiyo.

“Kutafuta suluhisho la ukosefu wa ajira kwa vijana ni miongoni kwa vipaumbele katika uongozi wangu wa kisiasa, lakini napenda kuona wananchi wanaishi kwa umoja na mashirikiano,” alisema.

Alisema kuwa zipo njia nyingi za kuwakomboa vijana kutokana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kuajiriwa katika viwanda vidogo vidogo na vya kati kupitia kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda, pamoja na kuwaelekeza kujishughulisha na uvuvi wa bahari kuu.

Eneo jengine alilolitaja kuweza kuwasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira ni sekta ya kilimo ambayo itawasaidia wananchi wengi kwa wakati mmoja kuondokana na tatizo hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment