WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 10, 2013

Wabunge waweka tofauti zao Bunge la Katiba

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe
 Wabunge jana waliandika historia mpya baada ya kuweka tofauti zao pembeni na kuunga mkono kwa kauli moja Mapendekezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, ambayo pamoja na mengine, yameongeza idadi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka 166 hadi 201 kutoka nje ya wabunge na wawakilishi.
Wajumbe hao, ambao watatoka katika makundi na taasisi mbalimbali za kijamii, watateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar kwa kuzingatia uwakilishi kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Mapendekezo ya Muswada huo uliopelekwa bungeni kwa hati ya dharura, yaliwasilishwa bungeni jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe.

Pia yamefuta utaratibu uliopitishwa awali wa maamuzi ya Bunge Maalumu la Katiba kufanywa na idadi ya wingi wa kawaida (simple majority) wa wajumbe.

Badala yake, maamuzi ya Bunge hilo linalotarajiwa kuanza mwezi ujao, sasa yatafanywa na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Muswada huo pia umependekeza kuweka kiwango cha chini na cha juu cha idadi ya watu wanaopendekezwa kwa ajili kuteuliwa na Rais.

Pia umependekeza kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi kufanya maandalizi yote muhimu kwa ufanisi wa Bunge Maalumu la Katiba.
Mapendekezo ya Muswada huo, yaliungwa mkono na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kupitia maoni yake yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pindi Chana.

Pia uliungwa mkono na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupitia maoni yake yaliyowasilishwa na Msemaji wake wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, licha ya kubainaisha kasoro kadhaa.

Vilevile, yaliungwa mkono na wabunge; Mohammed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF), Amina Makilagi (Viti Maalumu-CCM), Kombo Khamis Kombo (Mgogoni-CUF), Margareth Mkanga (Viti Maalumu-CCM), Jenista Mhagama (Peramiho-CCM), Freeman Mbowe (Hai-Chadema), John Mnyika (Ubungo-Chadema), William Ngeleja (Sengerema-CCM), William Lukuvi (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Uratibu na Bunge).
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment