WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 7, 2013

YANGA YAUA 3-0 NA KUPAA KILELENI LIGI KUU BARA, AZAM 3-3 NA MBEYA CITY CHAMAZI



Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
 
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Azam FC ikitoka sare ya 3-3 na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika 23, Mrisho Ngassa dakika ya 23 na Jerry Tegete dakika ya 53.
 
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupata bao kupitia kwa Humphrey Mieno dakika ya 13 na Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Mwagane Yeya 'Morgan' dakika ya 30.
ngassaa_4d5d4.jpg
Ngassa ameifungia Yanga Taifa leo
Mabao yote yalitokana na mipira ya pembeni, Mieno akifunga kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Farid Mussa nje kidogo ya 18, kufuatia kipa David Burhan kudakia nje ya eneo lake na Mwagane aiunganisha krosi ya Deus Kaseke.(P.T)

Kipindi cha pili, Mbeya City walitangulia kupata bao dakika ya 52 Mwagane Yeya tena akiunganisha kwa kichwa krosi ya Steven Mazanda, lakini John Bocco 'Adebayor' akaisawazishia Azam dakika ya 60 akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.
 
Mwagane tena akaifungia Mbeya City kwa shuti kali dakika ya 73 baada ya pasi ya Mazanda, lakini Khamis Mcha 'Vialli' aliyetokea benchi aliisawazishia Azam dakika ya 83, dakika tatu tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Farid Mussa.
 
Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 28 na kupaa kileleni, wakati Azam inashuka nafasi ya pili kwa pointi zake 27 sawa na Mbeya City, lakini inabebwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
 
Azam; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Salum Abubakar, Kipre Tchetche, John Bocco/Joseph Kimwaga 72, Humphrey Mieno na Farid Mussa/Khamis Mcha dk80.
Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda/Alex Sethi dk90, Paul Nonga/Francis Castor, Deus Kaseke na Richard Peter/Peter Mapunda dk46.
source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment