WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 12, 2013

DK MVUNGI AFARIKI DUNIA
Marehemu Dk. Sengondo Mvungi  enzi za uhai wake.
Marehemu Dk. Sengondo Mvungi alipokuwa ICU katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Habari za kusikitisha zilizotufikia jioni hii zinasema kuwa Dk. Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 mwaka huu kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea…

Marehemu Dk. Sengondo Mvungi  enzi za uhai wake.
Marehemu Dk. Sengondo Mvungi alipokuwa ICU katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Habari za kusikitisha zilizotufikia jioni hii zinasema kuwa Dk. Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 mwaka huu kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Muhimbili kitengo cha MOI ambako muda wote alikuwa hajitambui baada ya kushambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya sehemu ya kichwani akiwa nyumbani kwake Kibamba. Wakati Dk. Mvungi anafariki, jana Jeshi la Polisi, kupitia  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, lilitangaza kuwakamata watuhumiwa 9 wakiwa na mapanga yaliyotumika katika uvamizi huo.
Mpaka mauti yanamfika, Dk. Mvungi alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB).
Marehemu aliwahi kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMEEN!

source: Global publisher

No comments:

Post a Comment