WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 14, 2013

Kikwete: Ni taarifa iliyonisumbua na kunipa huzuni nyingi

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, nyumbani kwa marehemu Dk. Sendogo Mvungi, Mpiji Magohe, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.(PICHA:OMAR FUNGO)
Rais Jakaya Kikwete, ameeleza kushtushwa na kufadhaishwa na taarifa za kifo cha Dk. Senkondo Mvungi, akieleza kuwa ‘ni taarifa iliyomsumbua na kumpa huzuni nyingi.’
Katika taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kwa vyombo vya habari ikiwa ni salamu za rambirambi ambazo amemtumia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph SindeWarioba, ilisema Rais Kikwete amepokea kwa mshtuko mkubwa na fadhaha taarifa za kifo hicho.

Rais Kikwete alisema hakuna shaka kuwa katika maisha yake, Dk. Mvungi alitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa namna mbalimbali na kuwa kifo kimemfika wakati nchi ilikuwa inahitaji busara, hekima na mchango wake katika mchakato mzima wa kusaka Katiba mpya.

Alisema Dk. Mvungi ametoa mchango mkubwa kwa taifa kuanzia alipokuwa mwandishi wa habari katika magazeti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uhuru na Mzalendo, Uhadhiri wake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wakili katika Kampuni ya South Law Chambers, hadi uongozi wake katika Chama cha NCCR-Mageuzi.

Pia uamuzi wake wa kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2005 na sasa akiwa Mjumbe wa Tume ya Katiba, alitoa mchango wake mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu na kwamba hatasahaulika.

“Kwa masikitiko makubwa, nakutumia wewe Jaji Joseph Warioba, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu nikiombeleza kifo cha Dk. Mvungi, nakupa pole nyingi wewe Mwenyekiti, wajumbe wa Tume na wafanyakazi wote wa Tume kwa kuondokewa na mwenzenu, naungana nanyi kuombleza msiba huo mkubwa,” alisisitiza.

Rais Kikwete pia ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na majirani kwa kuondokewa na mhimili, msimamizi wa familia na ndugu na kwamba yuko nao katika msiba huu mkubwa.

“Msiba wao ni msiba wangu pia, binafsi naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu na namwomba Mwenyezi Mungu awape subira waweze kuvuka kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake,” alisema Rais Kikwete.

 “Napenda kuungana nao katika kumwomba MwenyeziMungu, Mwingi wa Rehema, aiweke mahali pema roho ya Marehemu Dk. Sengondo Mvungi. Amina,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment