WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 21, 2013

Simba wapewa siri ya Mzungu


Kocha Zdravok Logarusic. 

Logarusic aliwahi kuinoa Gor Mahia ambayo Mapunda anaidakia mpaka sasa.
Dar es Salaam. Kipa wa Taifa Stars na Gor Mahia ya Kenya,Ivo Mapunda amewaonya wachezaji  wa Simba wenye tabia ya uzembe kwa kuwataka wabadilishe mienendo yao vinginevyo watakabiliwa na hasira za Kocha wao mpya, Zdravok Logarusic.
Uongozi wa Simba juzi ulimtangaza Logarusic raia wa Croatia kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Abdallah Kibadeni aliyefungashiwa virago na aliyekuwa msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Logarusic aliwahi kuiona Gor Mahia ambayo Mapunda anaidakia mpaka sasa. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mapunda alisema Simba imelamba dume kumtwaa kocha huyo ambaye alimwelezea kama mtu mwenye msimamo na asiyependa masihara kwenye kazi.
“Mimi niwapongeze Simba kwa kumchukua Logarusic kwani ni kocha mzuri najua hata wao wamemchukua baada ya kuvutiwa na rekodi zake.
Julio aridhia na kudai chake Simba
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema amepokea kwa mikono miwili uamuzi wa kumfuta kazi uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo. 
Kamati ya Utendaji ya Simba juzi ilitangaza kumtimua Julio pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni ‘King’ kutokana na kile ilichodai kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao.
Mbali na kuwaondoa Julio na Kibadeni,kamati hiyo pia ilimsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage baada ya kumtuhumu kukiuka katiba ya klabu hiyo.
Julio alisema,“mimi na mwenzangu tumeupokea kwa mikono miwili uamuzi wa kutufukuza kazi, kama wao walituita na kuingia mikataba na sisi ili tuifundishe Simba  na leo wameamua kuivunja sidhani kama kuna tatizo hapo, jambo la msingi mimi nipate haki zangu tu.
Naye Kibadeni alisema hana pingamizi na uamuzi uliofanywa na kamati hiyo dhidi yake.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment