WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, November 8, 2013

Mvungi mahututi Jo’burg


Hali ya afya ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi aliyelazwa katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika Kusini inaelezwa kuwa ni mahututi.

Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia akizungumza jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Katiba alisema, kutokana na hali ya mjumbe huyo kuwa mbaya, aliwaomba Watanzania kuendelea na sala kwa ajili yake.(P.T)

Mbatia alisema, "Kwa kuwa tunazungumzia suala la katiba huku mmoja wa wajumbe wake Dk Mvungi ni mgonjwa, tunahitaji kufanya mchakato huu kwa kuweka mbele masilahi ya taifa.

"Hali yake Dk Mvungi bado ni mbaya sana huko katika hospitali ya Millpark na anahitaji kuombewa, hivyo Watanzania wote tumwombee," alisema Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Mwananchi lilipata taarifa kutoka katika hospitali hiyo ambapo kitengo cha ICU kilithibitisha kuwa hali ya Mvungi siyo nzuri na sasa yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Daktari wa kitengo hicho ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake alisema, wanaendelea kufanya kila mbinu za kitaaluma ili kuokoa maisha ya Mtanzania huyo.

"Tunafanya kila tuwezalo kumwondoa katika hali hii kwa sababu ameumia zaidi katika mishipa ya fahamu. Tunajitahidi," alisema.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema wizara inafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Dk Mvungi ingawa hawezi kusema chochote kwani suala hilo lipo mikononi mwa familia.

Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment