WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 3, 2013

DK.SENGONDO MVUNGI AVAMIWA, ACHARANGWA MAPANGA

Dr-Sengondo-Mvungi-e1305356005753_39a7a.jpg

Na Happiness Katabazi
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchi na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo(UB), Dk.Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana na kumacharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk.Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk.Mvungi, Dk.Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwai kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa.(P.T)

Dk.Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwaajili ya kuanza kupewa matibabu.

Binafsi habari hizi nimenishtua na zimeniumiza sana na kujikuta nalia usiku wa manane na ninaiomba serikali iwasake watu hao na iwafikishe katika vyombo vya sheria. Mara ya mwisho kuonana na Dk.Mvungi 'Rais Mdhulumiwa' ilikuwa Jumanne iliyopita ambapo nilienda ofisini kwake saa 12 asubuhi ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba ,ambapo nilikuwa na mdogo wangu Michael Machale ambapo tulizungumza mambo mengi sana kwa zaidi ya saa tatu.

Sina cha kueleza zaidi ila napenda kusema kuwa Dk.Mvungi ambaye amekuwa akipenda kuniita jina la utani ' First Lady' kwa sababu kuwa endapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 angeshinda nafasi ya urais , mimi ndiye ningekuwa mkewe na mimi hupenda kumtania kwa kumuita jina la utani 'Rais Mdhurumiwa' kwa maana kuwa mpinzani wake Rais Kikwete alimuibia kura za kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, na hivyo kusababisha mimi nisiwe First Lady ni mtu wangu wa karibu sana na nimiongoni mwa wazee wangu ambao wamekuwa wakinishauri mambo mengi hasa suala zima la kwenda kusomea kozi ya sheria na amekuwa akinichukulia kuwa ni mmoja wa watoto wake katika familia yake.

Itakumbukwa kuwa mimi nilikuwa ni mwandishi wa habari wa kike peke yangu kati ya waandishi wa habari wanne wa kiume ambao tulizunguka nchi nzima na Dk.Mvungi katika kampeni za yeye kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 2005.

Pole mke wa Dk.Mvungi, Anna, watoto wake ambao nawaita wanangu Dk.Natujwa, Nakundwa,Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia,NCCR MAgeuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Costa Mahalu,UB na watu wengine wote ambao ni watu wa karibu wa Dk.Mvungi.

Nakuombea Dk.Mvungi 'Rais Mdhurumiwa'upone haraka ili urejee tena katika kazi za ujenzi wa Taifa.
Imeandaliwa na 'First Lady' wa Dk.Mvungi, Happiness Katabazi
source: Mjengwa blog

No comments:

Post a Comment