WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, May 19, 2014

TASWIRA YA NYUMBANI KWA MAREHEMU ADAM KUAMBIANA SASA HIVI BUNJU!!

Mwili wa Adam Kuambiana ukiandaliwa tayari kwa kuagwa nyumbani kwake Bunju B jioni hii.
Waombolezaji wakiwa msibani tayari kuaga mwili. Wa tatu kutoka kulia waliokaa mbele ni mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi, Dar.
Watangazaji Sauda Mwilima (kulia) na Zamaradi Mketema (kati) wakiwa msibani hapo. Kushoto ni msanii Shamsa Ford.
William Mtitu (katikati) akiwa na waombolezaji.
Ibada ya kumuombea marehemu ikiendelea.
Mwili wa marehemu Adam Kuambiana ukitolewa kwa ajili ya kuagwa.
Baadhi ya wasanii baada ya kuwasili Bunju B.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani Bunju B.
Mwili wa marehemu ukishushwa kutoka kwenye gari Bunju B.

MWILI wa mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Kuambiana umeagwa nyumbani kwake Bunju B, Dar ambapo ndugu, jamaa, wanasiasa, marafiki wameshiriki tukio hilo. Kesho asubuhi mwili utapelekwa Viwanja vya Leaders kuagwa na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

(PICHA NA GABRIEL NG'OSHA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHAN / GPL)

chanzo:blog ya mwananchi

No comments:

Post a Comment