WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, May 31, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA KUHUSU CHANZO CHA AJALI ILIYOPELEKEA KIFO CHA DIRECTOR GEORGE TYSONNa. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi.
Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea  katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo chake.  Pia watu watano walipata maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa. 

Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.
Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWONGOZAJI WA FILAMU, Mkazi wa mbezi DSM. 


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu.  

Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-

1.   NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2.   GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3.   NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4.   JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI

Uchunguzi wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi. 

Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo wa kasi


CHANZO: MATUKIOTZ.COM

No comments:

Post a Comment