WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, May 10, 2014

Baraza Kivuli latangazwa

  Ni Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi
  Vyama vya TLP, UDP wawekwa kando

Baraza jipya la Mawaziri kivuli wa kambi ya Upinzani Bungeni lililotangazwa jana mjini Dodoma likiongozwa na kiongozi wa kambi hiyo Bungeni Freeman Mbowe wa sita kutoka kushoto. PICHA: TRYPHONE MWEJI
Umoja wa Katiba ya Wananchi Bungeni (Ukawa) umetangaza Baraza la Mawaziri vivuli kutoka vyama vya Chadema NCCR-Mageuzi na CUF.
Baraza hilo lenye   mawaziri 25 kutoka Chadema ,  11 wabunge wa  CUF na  wanne kutoka NCCR Mageuzi, lililowaweka pembeni wabunge wa  TLP na UDP,lilitangazwa jana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni , Freeman Mbowe  katika mkutano na wanahabari.

Akitangaza Wizara hizo, mawaziri na manaibu wao, Mbowe alisema Ofisi ya Rais(Utawala Bora), itaongozwa na Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema).

Ofisi ya Rais(Menejimenti na Utumishi wa Umma), Waziri ni Vicent Nyerere (Chadema).

Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Waziri ni Esther Matiko (Chadema), Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Waziri ni Mchungaji Israel Natse (Chadema) na Naibu wake ni Assa Othman Hamad (CUF).

Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Waziri ni Pauline Gekul (Chadema), Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Rajab Mohammed Mbarouk (CUF), wakati Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Waziri wake ni David Silinde.

Nyingine ni Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika, Waziri wake ni Meshack Opulukwa (Chadema) wizara hizo hazina manaibu.

 Wizara ya Nishati na Madini, itaongozwa na John Mnyika na Naibu wake, Raya Khamis Ibrahim wote kutoka Chadema,Wizara ya Fedha na Uchumi, itaongozwa na James Mbatia (NCCR Mageuzi) na naibu wake ni  Christina Lissu (Chadema).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, waziri kivuli ni  Ezekiah Wenje (Chadema) na naibu ni  Haroub Mohammed (CUF).

Wizara ya Katiba, Sheria na Muungano, itasimamiwa na Tundu Lissu (Chadema) na   Rashidi Abdallah (CUF) atakuwa naibu.

Nyingine ni Wizara ya Ujenzi, Waziri wake ni Felix Mkosamali (NCCR Mageuzi), Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Magdalena Sakaya (CUF) wakati Wizara ya Uchukuzi, itaongozwa na  Moses Machali (NCCR Mageuzi) wizara hizo hazina manaibu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wake ni Godbless Lema (Chadema) na naibu wake ni Khatibu Saidi Haji (CUF).

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, waziri wake ni Halima Mdee (Chadema) na pia haina naibu. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Waziri ni Rose Kamili (Chadema), akisaidiwa na  Mkiwa Adam Kiwanga (CUF).

Wizara ya Maliasili na Utalii, waziri wake ni Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kadhalika hana naibu.

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itaongozwa na  Joseph Selasini (Chadema), naibu wake ni Rukia Ahmed Kassim (CUF).

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  itakuwa chini ya Masoud Abdallah Salim (CUF) ambaye hana msaidizi. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, waziri wake ni Susan Lyimo na naibu wake Joshua Nassari wote kutoka Chadema.

 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, itaongozwa na Dk. Gervas Mbassa na  naibu  Conchesta Rwamlaza wote wa Chadema. Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, David Kafulila (NCCR-Mageuzi).

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia itaongozwa na Habib Mnyaa (CUF) na naibu wake Lucy Owenya (Chadema).

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, waziri wake ni Barwany Salum Khalifan (CUF) akisaidiwa na Sabreena Sungura (Chadema).

Wizara ya Kazi na Ajira, waziri wake ni Cecilia Paresso (Chadema). Haina naibu. Wizara wa Habari, Vijana na Michezo, waziri wake ni Joseph Mbilinyi (Chadema).

Awali akizungumza kabla ya kutangaza baraza jipya, Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alisema  baraza hilo litatoa taswira ya Ukawa ingawa tafsiri ya umoja huo ilionekana kwenye Bunge Maalumu la Katiba zaidi.

“Ushirika wetu, ulikuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba lakini sasa tunauleta ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.,” alisema.

Alisema uteuzi wa mawaziri hao ulifanywa kwa makini na kila mbunge ana zosifa na uwezo wa kuwa waziri hivyo haukuwa na upendeleo.

Kwa mujibu wa Mbowe, awali Baraza hilo lilikuwa dogo kwa vile lilikuwa la chama kimoja na hivyo kwa sasa wamebadilisha Baraza na kwamba wajibu wa mawaziri hao ni kuwakabili wale wa CCM.

Mbowe alisema mawaziri kamili wa CCM wapo 28, wa upinzani wapo 28 huku manaibu mawaziri wa CCM wakiwa 22 na wale wa upinzani wapo 12.

OMBI LA PINDA KURUDI BUNGE LA KATIBA

Kuhusu ombi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda la kurudi katika Bunge Maalum la Katiba, alisema hawezi kurudi  bali watahakikisha wanapambana nje ya Bunge hilo kwa kuwaeleza wananchi.

“ Unajua tunakabiliana na Chama kinaitwa Mbugi,Mbugi ni mchezo fulani wa mpira wa miguu wala hauna idadi ya wachezaji wala  muamuzi , we ukifika unangalia tu niingie katika timu iliyovaa fulana au iliyovua fulana basi unaingia kucheza, ukiona timu hii imefungwa unahamia kwingine ndiyo mchezo huo sawa na CCM”, alisema Mbowe.

Mbowe alisema wanashangazwa Pinda kuwataka kurudi katika Bunge hilo, wakati juzi kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) ilikaa na kuamua hakuna suluhu na Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) bali  watapambana nao kwa wananchi.

Awali Waziri Mkuu Pinda WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, aliwasihi wajumbe wa UKAWAU kukubali meza ya mazungumzo ili kuona jinsi wanavyoweza kufikia maridhiano kwa kuondoa matusi, kejeli na kudharauliana na hivyo Bunge hilo kuendelea kwa umoja Agosti 05, mwaka huu.

*Dunstan Bahai na Jacqueline Massano,  Ashton Balaigwa na Salome Kitomari, Dodoma.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment