WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, May 31, 2014

PIGO NYINGINE BONGO MOVIE:GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA


George Tyson enzi za uhai wake.
George Tyson akimlisha keki Yvonney Chery ‘Monalisa’ wakati mtoto wao Sonia alipopata kipaimara.
NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuweka picha hiyo juu na kuandika maneno yafuatayo:
Monalisa akimnywesha kinywaji Tyson wakati wa kipaimara cha Sonia.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MPENDWA WETU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!


GARI ALILOPATA NALO AJALI DIRECTOR GEORGE TYSON

Muonekano wa Gari alilopata nalo ajali Director George Tyson.
Kwenye hii safari, George Tyson (kulia) aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
DJ Choka (kushoto), akiwa na marehemu George Tyson (kulia) wakiwa Dodoma enzi za uhai wake.
Marehemu George Tyson enzi za uhai wake.
Dj Choka ambae alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
PICHA/HABARI KWA HISANI YA DJ CHOKA

SOURCE: GLOBAL PUBLISHER

No comments:

Post a Comment