WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 29, 2014

RACHEL HAULE AMETANGULIA MBELE YA HAKI ALILIWA NA WENGI


Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
 PICHA: Makatab za GPL

MWILI WA RACHEL HAULE WAAGWA , IRENE UWOYA AZIMIA. PICHA HIZI HAPA

Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao. Angalia picha zikionyesha matukio ya mwili wa Rachel tangu akitolewa Muhimbili, kupelekwa Sinza na Leaders..........

Irene Uwoya akiwa amezimia 

RACHEL HAULE AZIKWA LEO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

 Aunt Ezekiel na Wema Sepetu wakiwa makaburini.
 Mchumba wa Marehemu Rachel, Saguda (katikati) akiwa na majonzi tele wakati wa mazishi ya mchumba wake
 Majeneza yenye mwili wa marehemu Rachel na Mwanae yakiletwa Katika makaburi ya Kinondoni leo
 Mchungaji akiendesha sala ya kusalia Miili ya Marehemu Rachel na Mwanae katika Makaburi ya Kinondoni
 Majeneza Yakiweka katika kaburi 
 Waombolezaji wakiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Rachel
 Bibi Wa Marehemu akiweka mchanga katika kaburi ya Mtoto wa Marehemu Rachel aliyefariki wakati akijifungua
 Mchumba wa Marehemu akiweka mchanga katika kaburi la Mchumba wake, Marehemu Rachel
 
Mwakilishi wa Kampuni ya Proin Promotions akiweka Shada la Maua wakati wa mazishi ya Marehemu Rachel Haule na mwanae yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni.
 Mwenyekiti wa Bongo Movie akiweka Shada la Maua katika kaburi la Rachel
Mchungaji akiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu Rachel Haule

1 comment: