WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, August 9, 2013

Tunawatakia Eid el Fitri Yenye Baraka

 


Leo Waislamu wa Tanzania wanaungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumaliza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Ni siku ya kheri na furaha siyo tu kwa Waislamu peke yao, bali pia kwa Watanzania wote. kama vyombo vingi vya habari vilivyo tangaza na kuandika ni utamaduni wa Watanzania kuungana pamoja kusherehekea sikukuu kama ya leo. Utamaduni huo hakika unakuza upendo na hali ya kuaminiana na kuvumiliana miongoni mwa waumini wa madhehebu mbalimbali katika taifa letu.
Mwezi wa Ramadhan umekwisha, lakini mengi tumejifunza katika mwezi huu; tulifurahia amani na utulivu uliopo, tulifurahia imani na unyenyekevu ulioonyeshwa siyo tu na waliofunga, bali pia hata wale ambao hawakufunga. Kipindi hicho kilituonyesha kuwa ikiwa binadamu anataka kubadilika kimatendo anaweza kufanya hivyo, si kwa mwezi mmoja tu bali katika maisha yake yote.
Sikukuu tuliyoisubiri sasa ndio imefika. Matumaini yetu sote ni kwamba yale mema yote tuliyojifunza na kuyatenda wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan yataendelea kuakisi maisha yetu ya kila siku, hasa kwa kudhamiria kuwa raia wema wa taifa hili ambalo tunalipenda. Ni vyema tujikumbushe muda wote kwamba Tanzania ni yetu sote bila kujali dini zetu, itikadi zetu za kisiasa, silika na hata mila na tamaduni zetu, sote tunapaswa tuilinde kwa sababu nchi hii ni mama yetu ambaye akitutoka hatuwezi kupata mama mwingine wa kuchukua nafasi yake. Hivyo ni wakati wa kutafakari vitendo vyetu na tujiulize nini tufanye kwa mustakabali wa nchi yetu.
Ni wakati ambao Watanzania wanapaswa waitafakari amani yao, utulivu wao na upendo wao kwa taifa lao, isiwe imani, amani wala utulivu wa woga, bali vyote hivyo viwe vinatokana na dhamira ya dhati tuliyonayo mioyoni mwetu katika kuijenga nchi yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kutupeleka tunakokwenda.
Ramadhan, Eid, Krismasi, Pasaka na sikukuu nyingi nyinginezo zipo kwa ajili ya mazingatio ya nyakati na matendo yaliyotendeka zama zilizopita, lakini sisi wa zama hizi pia tunayo mazingatio yetu, tunazo shida zetu na tunazo tafakuri zetu, hivyo ni lazima tutafakari na tuzingatie yale yanayotukabili kama mtu mmojammoja na kama taifa.
Tunapaswa tudhamirie kujiondosha kutoka katika hatua moja ya kimaendeleo na tuingie nyingine kwa sababu tunaamini kwamba mawazo na hata matendo ya binadamu siyo mgando, tunapaswa tudhamirie kubadilika kwa wema na tubadilike kwa kutenda yenye manufaa zaidi kwa mustakabali wetu kama taifa.
Vitendo vya wizi, ubadhirifu, ufisadi, uzembe na yote ambayo tunadhani yanaturudisha nyuma kimaendeleo tudhamirie kuyapiga vita, kwani hivyo ndivyo masomo yanayotolewa na nyakati yanavyopaswa kuendelezwa. Kinyume cha hivyo jana yetu inakuwa haina tofauti na leo wala na kesho, kila siku mambo yanakuwa yaleyale. Hakika hiyo si silika njema anayopaswa kujipamba nayo mwanadamu.
Tunapaswa tuache kutenda kwa mazoea, tutende kwa dhamira, kwamba tunafahamu fika kuwa tukitenda jambo fulani jema, matokeo yake ni kupata jambo jingine jema zaidi kwa sababu kila jambo katika maisha lina nyongeza au punguzo. Kwa kufanya hivyo, hapana shaka kwamba tutakuwa tunaongeza thamani ya maisha yetu.
kuwatakia sikukuu njema na yenye baraka tele.
source Mwananchi

No comments:

Post a Comment