WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, August 14, 2013

Neno La Leo;

mahusiano 86637
Ndugu zangu,
Mahusiano ni neno fupi lakini nyenye maana pana. Yaweza kuwa ya mapenzi, kirafiki, kindugu, kikazi na hata kimajiriani.

Na katika dunia hii, pesa haiwezi kusimama peke yake kama yenyewe, lakini, mahusiano yanaweza kusimama peke yake kama yenyewe, hata bila kutegemegea pesa.


Wanadamu tunapaswa kuyatunza na kuyadumisha mahusiano . Maana, mwanadamu ameumbwa ili ajenge mahusiano mema na wanadamu wenzake.
Pichani nimesimama na Salim ' Asas' Abri kwenye moja ya visima vya kijamii shambani kwake. Huyu ni mmoja wa rafiki zangu hapa Iringa ninakoishi.

Na kwa ukweli, Salim ndiye aliyenifanya mimi na familia yangu tuchague kuishi Iringa, maana, kabla ya kuja Iringa kutoka Sweden, mwaka 2003 nilifika Iringa kuona kama kuna uwezekano wa kuja kufanya kazi hapa na kama kubwa kabisa, kama kuna shule ambayo watoto wangu wangeweza pia kusoma. Shule yenye kutoa elimu ya viwango vyenye ubora wa Kimataifa na yenye mazingira mazuri ya kujifunzia.

Salim alikuwa Mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Iringa International School. Alipofahamu kutoka kwa Mwalimu Mkuu, kuwa nimekuja kuitembelea shule hiyo, basi, Salim, kama mwenyekiti wa bodi, na hata kama hatukuwahi kukutana, alichukua jukumu la kuniandikia email kunielezea zaidi juu ya shule hiyo na hata kunishawishi, mimi na mke wangu, kufanya maamuzi ya kuchagua Iringa na Iringa International School.

Hata hii leo, miaka kumi baadae, Salim na mimi bado tuna mahusiano ya kirafiki na kushirikiana kwenye kazi za kijamii ikiwemo kuchangia kazi hizo, hata kwa mawazo tu.

Naam, lililo jema kwa mwanadamu ni kudumisha mahusiano na si kuyabomoa.
Neno Fupi La Siku ya Leo; Mahusiano....

Maggid,
Iringa.


No comments:

Post a Comment