WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, August 19, 2013

Ngao ya Jamii yarudi Jangwani

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub akinyanyua juu Ngao ya Jamii muda mfupi baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga. 

Dar es Salaam. Yanga imeng’arisha nyota ya mwanzo wa msimu wa baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mechi ya kibabe kuwania Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jana, Dar es Salaam.

Shujaa mechi hiyo kwa upande wa Yanga alikuwa Salum Telela aliyefunga bao pekee mwanzoni mwa mchezo na kupeleka hoihoi nzito Mtaa wa Jangwani
Ushindi huo unaifanya Yanga kuweka rekodi ya kutwaa mara tatu taji hilo.

Ilianza kulitwaa mwaka 2001 walipoifunga Simba 2-1, mwaka 2010 wakiifunga tena Simba kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 0-0.

Azam ndiyo timu pekee haijawahi kutwaa taji kati ya zilizowahi kucheza mechi ya Ngao ya Jamii. Mwaka jana walifungwa mabao 2-1 na Simba, Mtibwa walikuwa washindi wa mwaka 2009 walipoifunga Yanga 2-1.

Kocha wa Azam, Stewart Hall alikubali matokeo hayo na kusema, timu yake ilipoteza mchezo huo baada ya kushindwa kuwa makini dakika tano za mwanzo za mchezo, na kuisifu Yanga kwa kusema ilicheza vizuri.
Kwa upande wake, kocha wa Yanga Ernest Brandts alikisifu kikosi chake na kusema kilicheza vizuri na pia amefurahi kuona wachezaji wake wanazidi kuimarika kila siku.

Iliwachukua Yanga dakika mbili tu kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Salum Telela aliyeunganisha mpira wavuni akimalizia kazi nzuri ya Didier Kavumbagu.

Katika mchezo huo, Yanga iliwakosa wachezaji wawili kutokana na kuumia, akianza beki Kelvin Yondan aliyeshindwa kuendelea na mchezo kufuatia kugongana na John Bocco na nafasi yake kuchukuliwa na Mbuyu Twite.

Kipa Ally Mustapha naye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Deogratius Munishi baada ya kuumia kwenye piga-nikupige langoni kwa Yanga katika dakika ya 19.

Azam nao walimkosa mshambuliaji wao Bocco aliyelazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Mwaipopo baada ya kugongana na Twite katika dakika ya 73.

Azam wangeweza kusawazisha katika dakika ya 30, kama siyo shuti kali la mshambuliaji, Kipre Tchetche kugonga mwamba wa Yanga na mpira kutoka nje, huku Jerry Tegete akipaisha juu shuti lake dakika ya 57

Telela naye alipoteza nafasi nzuri ya kuimarisha ushindi wa Yanga baada ya kupiga nje ya lango mpira kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Haruna Niyonzima.
Mchezo huo ulijaa ubabe na rafu zisizo na ulazima kiasi cha Twite kushonwa mdomoni baada ya kupigwa kiwiko na Gaudence Mwaikimba wa Azam, huku Aggrey Morris akimchapa kiatu Kavumbagu mshambuliaji wa Azam mwishoni mwa mchezo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik aliwakabidhi Ngao ya Jamii, mabingwa, huku George Mkuchika akiwavisha medali wachezaji wa Azam.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment