WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, February 13, 2014

Rais Kikwete amenawa mikono kazi kwenu wabunge

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ametangaza majina 201 ya wajumbe kutoka makundi mbalimbali nchini walioomba kuteuliwa ili waungane na wabunge wa Bunge la Jamhuri na la Wawakilishi Zanzibar waliopo, kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Kabla ya kutangaza majina hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Florence Turuka, alisema kazi ya kuwapata wajumbe wa Bunge hilo ilikuwa ngumu.

Kwa sasa Rais Kikwete amenawa mikono kama Pilato, na sasa analala usingizi mnono, akiwatazama wajumbe aliowatupia zigo ili wajadili mustakabali wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni wa nchi hii na ikitokea wakaboronga ni wao wenyewe lakini yeye nadhani hahusiki tena.

Kwa msingi huo huo, hatutarajii tuone tena kuna watu wanasinzia na kulala usingizi katika Bunge hili Maalum kama tulivyozoea kuwaona baadhi ya wabunge  wakipiga usingizi hadi wakafikia kukoroma na kutoa udenda mdomoni.

Aidha, hatutaki kuona tena, usingizi huu na kauli ya wanaoafiki waseme ndiyo hata kama mbunge alikuwa amelala na wala hakujua chochote kilichokuwa kikizungumzwa.

Utaratibu wa kuafikiana ufanyike kwa kupiga kura za siri ili kila mtu awe huru kupendekeza anachoona kinafaa badala ya kuulizwa kwa mdomo.

Pamoja na wabunge wa Bunge la Muungano na Wawakilishi kule Zanzibar, lakini macho na masikio ya watanzania nikiwamo mimi, kwa sehemu kubwa sana tunawaangalia na kuwategemea wajumbe  201 toka makundi mbalimbali, walioteuliwa ili wawe mawakili.

Walioteuliwa ni kutoka taasisi zisizokuwa za kiserikali, taasisi za kidini Tanzania Bara,  kundi la vyama vya siasa, taasisi za elimu, watu wenye  ulemavu, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wafugaji, vyama vya wavuvi, vyama vya wakulima na watu wenye malengo yanayofanana.

Kama kati ya watanzania zaidi ya milioni 44, wajumbe hao 201 wameteuliwa, ni matarajio yangu watathamini uteuzi huo, na hivyo katika mjadala huo wa rasmu ya pili ya katiba, watajikiti kuangalia mustabali na uzalendo wa taifa hili, ili waandike historia muhimu maishani mwao.

Naamini wajumbe hao watatamani kuandika historia katika maisha yao ili wakumbukwe na vizazi vya miaka 50 ijayo ambapo vizazi hivyo vitasoma, vitasikia, na kushuhudia katiba nzuri na kuwapongeza kuwa walifanya kazi nzuri na kusujudu makaburi yao badala ya kuwalaumu.

Lakini kama wajumbe hao watajadili usingizi wa Itikadi zao, dini zao, maslahi ya uongozi wa watu fulani binafsi, ukanda, ukabila bila kujali utaifa; vizazi vijavyo vitawalaumu kwa kutengeneza katiba mbovu.

Ikiwa katiba mpya haitapatikana kutasababisha msuguano mkubwa miongoni mwa jamii nchini Tanzania, kwa sababu iliyopo imeonesha mapungufu makubwa ambayo kwa namna moja au nyingine, imekuwa ikiwanyima haki wananchi na hasa wapiga kura.

Ni rai yangu wajumbe wafahamu kwamba, wanakwenda huko huku wakijua kuwa, kama watafanya madudu yasiyotarajiwa kutupatia katiba mpya, waelewe wananchi bado tuna nafasi ya kuipigia kura ya kuikataa ama kuikubali.

 0715933308


CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment