WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, February 9, 2014

CCM YASHINDA NAFASI YA UDIWANI KATIKA KATA YA NDULI KWENYE MANISPAA YA IRINGA

CHADEMA YAPIGWA CHINI, KATIKA VITUO TISA VILIVYOPIGIWA KURA, CCM IMESHINDA VITUO NANE WAKATI CHADEMA WAKIPATA KIMOJA TU KATIKA KATA YA NDULI KWENYE MANISPAA YA IRINGA.
FURAHA_12_22c07.jpg
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi katika kata ya nduli kwenye manispaa ya Iringa wakiserebuka na kuimba kwa furaha baada ya kupata taarifa ya ushindi wa chama cha mapinduzi katika ngazi ya udiwani, uchaguzi huo ulifanyika jana, siku ya jumaapili ya tarehe 9/2/2014 ambapo Bw. Bashiri Richard Mtove aliibuka mshindi na kumpiku mpinzani wake kutoka chama cha demokrasia na maendeleo Bw. Ayubu Abdalah Mwenda katika ngazi hiyo ya udiwani
FURAHA_7_46be0.jpg
Bw. Bashiri Richard Mtove akiwashukuru wanachama wake wa CCM waliomuwezesha kuibuka na ushindi katika kampeni hizo ziliofanyika katika kata ya nduli, jumla ya vituo vya kupigia kura vilikuwa tisa lakini CCM ilishinda katika vituo nane na kupoteza kimoja tu ambacho kilishikiliwa na CHADEMA; kituo cha Mibata ndicho kilichoongozwa na CHADEMA kwa jumla ya kura 103 wakati CCM ikipata kura 48 lakini katika vituo vingine vyote CCM walishinda kwa kishindo kikubwa na hata kuweza kunyakua nafasi hiyo dhidi ya wapinzani wao wakuu CHADEMA.FURARA_1_e216c.jpg
baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa katika shangwe na vifijo baada ya kupata taarifa ya ushindi dhidi ya CHADEMA, hili ni eneo la kituo cha mabasi ya kubeba abiria katika kata ya Nduli.
FURAHA_5_fb6f2.jpg
mwanachama mmoja wa CCM akitoa pongezi zake za dhati kwa Bw. Bashiri Richard Mtove aliyeibuka na ushindi wa udiwani katika kata ya Nduli; wanachama wa chama cha mapinduzi walijawa na furaha isiyo kifani na hata kupiga mayowe huku wakiwaimba wanachama wa CHADEMA kwa kushindwa kuipata nafasi hiyo ya udiwani wa kata hiyo.
FURAHA_3_0c58b.jpg
katibu wa CCM katika manispaa ya Iringa Bw. Hassan Mtenga akitoa shukhrani zake kwa wanachama waliojitolea kumpigia kura Bw. Mtove aliyekuwa anaiwakilisha CCM katika ngazi ya udiwani
FURAHA_10_7c940.jpg
baadhi ya watu waliokuwa wanaelekea katika kituo cha Godown ambapo ndipo ilikuwa sehemu kuu wanapotolea matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa diwani wa Nduli
CHADEMA_a8265.jpg
baadhi ya wanachama wa CHADEMA waliokuwa karibu na eneo hilo wakiondoka na kutokomea sehemu nyingine. wanachama hao wa CHADEMA hawakuonekana tena katika eneo hilo.
FURAHA_cb9b8.jpg
FURAHA_9_85a20.jpgpora_bb_08979.jpg
jeshi la polisi lililotakiwa kutuliza amani na utulivu lilifanya kazi yake kama ilivyo takiwa na hakukuwa na ugomvi wowote ule kwa kuwa hali ya ulinzi ilikuwa katika kiwango cha juu
20140209_190030_50ac5.jpg
furaha ilipitiliza mpaka wengine wakachoka na kuishia kukaa chini kwani waliimba na kucheza sana baada ya mwanachama wao kushinda nafasi hiyo ya udiwani
FURAHA_10_992ef.jpg
baadhi ya wanachama waliokuwa wakielekea katika kituo cha Godown ambapo matokeo yote yalikuwa yakitolewa kwa ujumla
pora_60883.jpg
kila mtu alishangilia kwa staili yake kwani ilikuwa ni furaha iliyopitiliza na kila mtu alicheza na kuimba kwa sauti; watu wa rika zote walikwepo kuanzia watoto mpaka watu wazima
FURAHA_15_9e27d.jpg
mitaa ya kituo cha mabasi ya abiria palikuwa ni kucheza tu kwani watu walijaa na kusherekea kwa furaha isiyo kifani kutokana na ushindi wa CCM FURAHA_4_46d88.jpg
mueshimiwa diwani alipobebwa na kundi ka wanachama wa CCM waliokuwa na furaha na hata kujidai kwa jitihada za chama chao; hivyo basi chama cha mapinduzi CCM ndicho kilichoibuka na ushindi kupitia mgombea wake Bw. Bashiri Abdalah Mtove.
imeandikwa na Riziki Mashaka.

SOURCE: MJENGWA BLOG

No comments:

Post a Comment