WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, February 3, 2014

HEBU TUTAFAKARI KWA KIFUPI SAFARI YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Leo tunaposubiri majina ya watanzania watakao tuwakilisha katika bunge la Katiba mpya 2014 hebu tujikumbushe tumefikaje hapa kwa ufupi?BUSARA ALIYOIONYESHA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE YA KUANZA KUKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA TUMEzIPOKEA KWA FURAHA KUBWA;

 “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 29, 2011, alitia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.  

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.”


Kama taifa inatupasa kukumbuka kuwa  mabadiliko ya katiba ni madai ya msingi na matakwa ya lazima kama nchi yetu kama inataka kujenga na kudumisha amani ya kweli na kuleta maendeleo kwa watu wake; wazo la serikali na vyama vya siasa na asasi zingine zinazojishughulisha kudai na kuhamasisha mabadiliko haya ya msingi kuendelea kutambuka kuwa  Safari hii  ya utungaji wa katiba ni ya Muhimu sana. 

Kutokana na umuhimu huu mkubwa kwa faida ya Taifa,hivyo ni wajibu wao  kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nafasi ya  kujua zaidi kuhusu mapungufu ya katiba ya sasa na nini kitarajiwe katika katiba mpya. Wananchi wapate nafasi ya kwanza katika kutoa mawazo ya nini wanataka wakati tume ya kukusanya maoni itakapowatembelea. Lakini kama watapuuzwa tutajenga ufa mwingine katika katiba mpya.

Je vyama vya siasa na asasi zake kwa sasa hivi zimeandaa mikakati gani ya kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia maoni?

Tatizo nilionalo mimi kama vyama vya siasa  vitaendelea kulumbana vyenyewe vifahamu kuwa havina nafasi ya kumsaidia mwananchi wa katika kujinasua katika hali duni kwani katiba na utungaji wake vitabaki kuendelea kumilikiwa na wanasiasa na wasomi na wanjanja wachache.


Tukiangalia wenzetu kama Marekani pamoja na  uwezo wao  na maendeleo yao bado Katiba ni chombo cha wananchi na sio chombo cha chama Fulani, na katiba yao imejengwa katika msingi mkubwa sana wa uhuru ambao umewekwa katika katiba yao. Ikiongozwa na maneno haya " We The People"
Jukumu la wanasiasa kuwaelimisha wananchi kuhusu marekebesho ya  kutungwa kwa katiba mpya ni la muhimu sana kwani wananchi wengi  hawajui katiba ya zamani ina matatizo gani, hivyo wasipoelimishwa hata mabadiliko yanayokusudiwa hayatakuwa na msisimko wowote kwao na katiba mpya haitakuwa na maana yeyote kwao.  
Kwa serikali vyama vya upinzani na Asasi zinazojihusiha na maswala ya katiba, tunaviomba sana katika mchakato huu mzima wa uandikaji wa katiba mpya  vitumie nafasi hii vizuri kwa kujadiliana juu ya Katiba mpya, kwa kudumisha utamaduni wa kuvumilia pamoja na tofauti zao za vyama na mtazamo. itafurahisha sana kama wahusika wote watakuwa na mtazamo chanya na kutanguliza taswira nzuri ya Taifa kwa masilaha ya wananchi wote bila kubagua.
Nakumbuka  Profesa Shivji katika moja ya mikutano ya changamoto ya katiba mpya ya Tanzania aliwahi sema kuwa  “mchakato wa upatikanaji wa kabisa mpya ni fursa muhimu ya kurejesha mwafaka kwa majadiliano kuliko ilivyo sasa ambako kuna kila dalili za kuelekea katika magomvi na mapambano”


Kwa maneno mengine Professor Shivji  anatukumbusha kuwa Katiba inatakiwa iwe ni mali ya  wananchi, ndio wananchi  lazima wawe  wenye uamuzi wa aina ya serikali wanayotaka kuwa nayo na na namna itakavyo waongoza, wananchi ndio msingi wa madaraka yote nchini. Kwa maneno mengine Katiba inatakiwa itoke kwa wananchi. Siyo katika kuipigia kura tu bali katika uandikaji wake. Katiba ambayo haitoki kwa wananchi na haiweki ushiriki wa juu kabisa wa wananchi kutoka mwanzo haiwezi kudai kuwa ni katiba ya wananchi hao.

Kwa mtazamo wangu na wengine wengi ambao sio wanansiasa au wasomi  tunatamani kuwa Katiba Mpya iwe ni kumbu kumbu endelevu na kwamba, kasoro zilizojitokeza kiasi cha kutibua morari na hali ya watanzania, iwe ni changamoto ya kuwa makini zaidi katika mchakato mzima wa uandikaji wa Katiba Mpya, mzaha wowote unaweza kulitumbukiza Taifa katika maafa makubwa lazima usipewe nafasi kwani tunatamani katiba yetu iwe kama ile ya Merakani ambayo imesimama imara na inatekelezeka. 


Kama Mwalimu Nyerere alivyowahi sema katika moja ya mikutano yake kuwa  Katiba ni sheria mama, iguse msingi wa mambo makuu yatakayoongoza sheria, sera na mifumo ya kitaifa. Hii ni dhamana nyeti inayopaswa kuwashirikisha wataalam kutoka katika medani mbali mbali za maisha ya wananchi nchini Tanzania. 

Wanasiasa waepuke vishawishi na kudhani kwamba, wao ndio wanaopaswa kusimamia na kuongoza mchakato huu, wajitahidi kushiriki kama watanzania wengine kwa kuchangia mawazo yao na sio kuhozi katiba mpya kama mali ya chama chao.

Katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba tuzingatie

  • Katiba Mpya inapaswa kuwa ni mali ya watanzania wote kwa kuwa mchakato mzima unawashirikisha watanzania wengi zaidi kwa njia ya moja kwa moja au uwakilishi wao. Chombo kitakachopewa dhamana ya kusimamia kuandika Katiba Mpya, kwanza kabisa kikubalike na watanzania wengie, hii itakuwa ni hatua kubwa hata kuweza kuridhia kile kitakachoandikwa. Miongozo itolewe katika lugha inayoeleweka na fasaha ili kuwa na tafsiri sahihi na rahisi kwa watanzania wa kawaida kabisa·   Washauri wa mheshimiwa Rais tunawaomba wamshauri Rais wetu kwa kujali zaidi masilahi ya Taifa na sio vinginevyo wakizingatia kuwa serikali yetu kwa hivi sasa inaingia katika kipindi muhimu sana cha kulipitisha Taifa letu katika wakati huu kwa maendeleo ya wananchi wote na sio kikundi kidogo cha watu;
· Katiba yetu ikamilishwe kutungwa kwa majadiliano na makubaliano ya umoja wa kitaifa na sio kwa vitisho vya Migomo na maandamano na shinikizo la vyama kwa masilahi binafsi. 

·   ili kupata Katiba makini inayozingatia mafao ya wengi kuna haja kwanza kabisa kuwa na utulivu wa kimawazo, busara na hekima vitumike zaidi, kwa kuzingatia umoja wa kitaifa na upendo kati ya watu. Masilahi ya taifa yapewe kipaumbele cha kwanza na kamwe ubinafsi usiruhusiwe kutawala zoezi nyeti kama hili.·        Ebu tuache  malumbano wakati huu ni mzuri kwa vyama vya siasa tanaznia pamoja  asasi zanazojishughulisha na mambo ya  sheria kutumia muda huu kuwafundisha  wananchi katiba ya zamani na waone hayo mapungufu yake halafu wapate kutoa maoni  yanayolingana na mahitaji yao na sio kufuata mkumbu wa mahitaji ya wanasiasa kama inavyoendeleahivi sasa;

HITIMISHO;

Kwa msingi huu vyama vyote yaani  CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TLP na Vyama vingine vya siasa vikumbuke kuwa “Katiba ya nchi si mali ya chama au mtu binafsi na wala si mali ya kiongozi fulani, ni mali ya watu wote raia wa Tanzania na wala katiba isipatikane kwa shinikizo la kukundi chochote cha watu”


kama Dk Salim Ahamed Salim aliwahi sema kuwa “Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya. 

Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifaKwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa letu,”


kwa hiyo tunavyoelekea kupata katiba mpyaa ifikapo mwaka 2015 kama serikali ilivyohaidi, Tanzania kama nchi ambayo imeingia katika mfumo wa vyama vingi miaka ya 90, inahitaji mabadiliko au katiba mpya yenye misingi YA UPANA NA UWAZI WA DEMOKRASIA na misingi mipya ya kuongoza vyama vingi na mawazo mapya ya Jamii kwa msingi huu kama sisi kama Taifa tutafanikiwa kupata katiba mpya basi tukakuwa  tumejijengea  katiba  iwapo vile vile tutaweza kujumuisha kwenye uandikaji wa katiba mpya kwa maoni ya wananchi hapo tutakuwa tumejijengea  Utawala wa Demokrasia ya umma.


Tunaendelea kumpongeza mheshimiwa Rais kwa busara yake ya kuanza kukutana na vyama vya upinzani CHADEMA, katika kufikia muafaka na kushauriana katika kuboresha uandikaji wa katiba mpya; tunamwomba mheshimiwa Rais aendelee kukutana na wale wote wenye nia njema, katika kuboresha katiba yetu mpya;


MUNGU IBARIKI TANZANIA KATIKA MAANDALIZI YA KATIBA MPYA

No comments:

Post a Comment