WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, February 3, 2014

Kikwete: Wajumbe Bunge la Katiba kutangazwa leo, kesho

JK 7c762

Rais Jakaya Kikwete amesema uteuzi wa majina 201 ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba umekamilika na kati ya leo na kesho, atayatangaza pamoja na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo. (HM)

Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 90 kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana.

"Bunge la Katiba litakutana katika wiki ya tatu ya mwezi huu. Mambo yanayosubiriwa ni mawili tu, uteuzi wa wajumbe 201 na siku ya kuanza kwa Bunge hili. Mambo haya yote ninayesubiriwa kuyakamilisha ni mimi tu," alisema Rais Kikwete alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM.

Alisema kazi ya uteuzi wa wajumbe hao ilikamilika tangu juzi na kinachofanyika sasa ni kuhariri majina hayo na kurekebisha mambo kadhaa.

"Jumatatu (leo) tutayapitia majina haya ili tuone kama tunaweza kurekebisha. Baada ya hapo tutaweza kutangaza na inaweza kuwa siku hiyohiyo au kesho yake (Jumanne), hazitazidi siku hizi mbili," alisema.
Alisema hivi sasa ukarabati katika Ukumbi wa Bunge, Dodoma bado unaendelea na mkandarasi ameeleza kwamba hadi Februari 10, mwaka huu atakuwa amemaliza kazi.

"Nimewapa siku tano hadi saba za kujaribu spika na vipaza sauti ili kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, lakini pia nitakwenda kupata ushauri wa wanasheria ili kuweza kutangaza siku ya Bunge hili kukutana," alisema.

Amshangaa Mbowe

Katika hotuba yake Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kauli yake kwamba mfumo wa Serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo, nchi haitatawalika.

"Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa," alisema.

Alisema si kweli kwamba kila mwanaChadema anataka mfumo wa Serikali tatu na kila mwanaCCM anapendelea mfumo wa Serikali mbili akisema kinachohitajika ni ushawishi wa kujenga hoja ili wanaopinga wakubaliane. 

Chanzo: mwananchi

No comments:

Post a Comment