WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, September 7, 2013

Oh! Oh! Picha ya Aibu Hii.. Hivi Watanzania Tunapenda ' Vurugu mechi?!

bungeletu_db6c9.jpg
Ndugu zangu,
Hivi Watanzania ni watu wenye kupenda ' Vurugu Mechi'? Maana, magazetini leo habari kubwa na picha ni ' vurugu mechi' bungeni.
Ni picha ya aibu. Shabaan Robert alipata kuandika, tena miaka 50 iliyopita, kuwa isifike mahali wazungu wakarudi wakatukuta bado hatujamulikiwa na nuru, kwamba Waafrika bado tunapigana hadharani!(P.T)
Shaabani Robert alikuwa na maana ya kuwa hayo ni mambo ya kishenzi na hayapaswi kufanywa na watu wastaarabu.
Na afadhali wasomaji wa magazeti kwa lugha ya Kizungu leo hawakuonyeshwa picha za sisi Waafrika tulivyo hata baada ya miaka 50 ya uhuru. The Citizen na Daily News wao walipamba sura za mbele za magazeti yao kwa habari kubwa ya JK na PK ( Kikwete na Kagame) walivyokutana Kampala jana.
Habari za aibu ya bungeni zilipewa nafasi ya pili tena bila picha. Pongezi kwa wahariri wa magazeti hayo kwa kutufichia aibu yetu.
Na Daily News wao wametoka na kichwa kizuri cha habari; " MPs, police in a shameful flurry of fists"
Kwa kweli ni aibu. Kwa nini tumefika mahali hapa? Kwamba watu wazima Bungeni wasitumie mazungumzo katika kumaliza tofauti zinazojitokeza badala ya kushikana mashati, kuburuzana na hata kupigana makonde.
Na mitaani leo kona nyingi nimewasikia watu wakizungumzia ' Senema ya jana Bungeni'. Na kilichowavutia sana ni hiyo ' Vurugu mechi' na hususan masumbwi na kupigana ngwala!
Na wengi hawakujikita kwenye nini hasa msingi wa vurugu mechi hiyo. Wamefurahishwa tu na ' Vurugu mechi', basi! Na hakika, magazeti yaliyopambwa na picha za vurugu mechi ile leo yameuzwa ' kama njugu'.
Na bwana mmoja mtaani nimemsikia akitamka; " Sasa tunataka kuona masumbwi ya wabunge wa upinzani dhidi ya wa CCM!"
Tumefika pabaya, kwamba habari za aibu za watu wazima kupigana na kushikana mashati hadharani ndizo zinazowavutia wasomaji watu wazima!
Hivi watoto wetu tunawafundisha nini?
Kwamba katika nchi hii unaweza kuwa maarufu na hata ukafika mbali kwa kurusha ngumi badala ya kuwa na uwezo wa kujenga hoja kwa kutumia kichwa, mdomo au kalamu.
Si tunajua, tuna hata mwanasiasa katika nchi hii aliyerumshia ngumi mwanahabari hadharani, na tangu siku hiyo akajipatia umaarufu na hata kupewa jina la ' Tyson'!
Ndio, ni katika nchi zetu hizi za hovyo hovyo ambapo ngumi zinaweza kukupeleka hata IKULU!
Usiku Mwema.
Maggid.
Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment