WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, July 20, 2013

Nyerere: Serikali corrupt haikusanyi kodi - Sehemu ya hotuba “Nyufa”


Nguvu ya kudai kodi kwa Wamachinga, Wenye magenge, SIMCard, Wafanyakazi n.k. VERSUS nguvu ya kudai kodi kwa mfano:
  1. Raia wa kigeni akwepa kulipa kodi kwa miaka 8 - Habarileo Julai 20, 2013
  2. Serikali imewekwa mfukoni na Said na Ghalib Saad wa Home Shopping Center? - Rai 2010
  3. Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center - JamiiForums, 2012.

'All animals are equal, but some animals are more equal than others,' Animal Farm, book by George Orwell.
Nazungumza habari za kutokusanya kodi. Kutokusanya kodi ni sifa moja ya viserikali corrupt popote pale. Popote, wala usifikiri ni Tanzania peke yake, au Kenya peke yake... Italy pale. Italy, serikali iliyotoka hii wana mzigo wa madeni. Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali. Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambieje mwenye mali, kwamba “utalipa, uspolipa utakiona!" Atacheka tu huyu. Atakwambia “unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!”

Serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi. 

Nukuu ya sehemu ya alichokisema hayati Mwl. Julius K. Nyerere, kuanzia dakika ya 16:32. 
Hotuba nzima imepachikwa hapo chini (youtube video).
Miiko ya Uongozi — Zamani tulikuwa na kitu kinaitwa miiko ya uongozi wakati wa TANU, zilikuwa zinaitwa Kanuni za TANU. Na kanuni moja ya TANU, ambayo baadaye tukarithi katika CCM au tukairithisha CCM, inasema; “Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa”.

Usije ukadhani kwamba wakati wa awamu ya kwanza palikuwa hapana rushwa; ilikuwapo, lakini tulikuwa wakali sana. Siku za mwanzo kabisa, tulitaka watu wajue hivyo. Tulitaka watu watu wajue kwamba tutakuwa wakali sana na wala rushwa ndani ya serikali na wale wanaotoa rushwa. Mwanzo kabisa wakujitawala tulitaka kila mtu ajue. Tukapitisha sheria kwamba mtu akila rushwa, eh! Kiongozi wetu anakula rushwa: anayetoa, aliyepokea, Wazanaki wanasema manzi ga nyanza yaani, wote wanapata msukosuko.

Rushwa! Sasa Tanzania inanuka kwa rushwa. Ufa mwingine tulioupata. Tunataka kiongozi anayejua hivyo ambaye atasema “rushwa kwangu ni mwiko.” Mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na wanamjua watoa rushwa: watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu. Maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu. Mambo haya yana matatizo. Unaweza ukawa wewe mwenyewe mwaminifu kabisa, safi kabisa, lakini una presha za ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako. Kwa hiyo, sio kwamba inatosha wewe uwe mwaminifu tu, bali uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa na rafiki zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena, IKULU NI MAHALI PATAKATIFU. Unawaambia ngu zako na jamaa zako na marafiki zako firmly kabisa kabisa ‛Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi.” Ukishakuwaambia hivyo ndugu na rafiki zako na ikajulikana hivyo, mtu wala hakusogelei. Nafsi yake haimtumi kukusogelea.

source: wavuti.com

No comments:

Post a Comment