WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, July 8, 2013

Dk.Ali Mohamed Shein, na Dk.Salmin Amour Juma Waung'uruma Kwenye Mkutano wa CCM kibanda Maiti Zanzibar

 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Komandoo) Dk.Salmin Amour Juma, alipokuwa akiwasalimia na kuwahutubia katika Mkutano wa hadhara Kibanda maiti Mjini Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar.
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja,katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar,katika mkutano huo ulizungumzia uwepo wa Serikali mbili kwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania.
 Mzee Ali Ameir akisalimia na kutowa Salamu za Wananchi  katika mkutano huo
Mwenyekiti wacCCM Mkoa wa Mjini Silima Borafya akizungumza katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa ccm Zanzibar Vuai Ali Vuai, akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti Unguja na kuhudhuriwa na Wanachama wacCCM wa Mkoa Minne ya CCM Unguja.
 Wanachama wa CCM wa maskani ya Kisonge wakishangilia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Uwanja wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.
 
Kombando Dkt. Salmin Amour Juma, akiwasalimia wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti Zanzibar. hii ni mara ya kwanza kwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar kuhutubia katika hadhara kama hii na kushangiliwa na Wananchi na Wanachama wa CCM waliokuwa katika viwanja hivyo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia Mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya Kibanda maiti.
Komandoo Dkt. Salmin Amour Juma akiwasilimia Wanachama wa CCM katika viwanja vya Kibanda maiti.
 Wanachama wa CCM wakishangilia katika mkutano huo
Mwananchi akichukua picha kupitia simu yake wakati wa mkutano wa hadjara wa CCM.


 
 
 
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti Unguja.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Alhaj Mwangi Ramadhani Kundiya, akisoma risala ya WanaCCM wa Mkoa Minne ya Unguja katika mkutano huo uliohutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika viwanja vya Kibanda Maiti. 
source Haki ngowi & ZanziNews

No comments:

Post a Comment