WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, July 3, 2013

MICHELLE OBAMA AMFAGILIA MAMA SALMA KIKWETE

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama pamoja na Mama Laura Bush, mke wa Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush kwenye hoteli ya Serena tarehe 2.7.2013.
---
Na Anna Nkinda - Maelezo 
Mke  wa Rais  wa Marekani  Mama  Michelle Obama amempongeza  Mke wa Rais  Mama  Salma  Kikwete  kwa kazi  kubwa anayoifanya  ya kutoa elimu bure  kwa watoto Wa kike ambao ni yatima  na wanaoishi katika mazingira hatarishi .

Mama Obama  alizitoa pongezi hizo leo wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa   wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena  jijini Dar es  Salaam.

Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia  wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.

"Jana nilitembelea  makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto  ambao  baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika 
ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya,  elimu na ujasiriamali.

Mama  Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi  na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara  la Afrika.

Mkutano huo wa siku mbili   umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya  kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihojiwa na Mtangazaji, Adesewa Josh kutoka  Channels TV ya nchini Nigeria wakati wa mkutano wa wake wa Marais wa nchi zaa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam tarehe 3.7.2013.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika wakisikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipohutubia mkutano huo tarehe 3.7.2013.Picha na John Lukuwi
source: Haki Ngowi

No comments:

Post a Comment