WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, July 2, 2013

mr president vipi uwekezaji katika soka la bongo?


ob9 8750b

Heshima kwako mheshimiwa Rais wa 44 wa Taifa kubwa duniani  la USA ,Ndugu Barack Hussein 

Obama, awali ya yote nilifurahishwa na maandalizi ya ujio wako na furaha ikatimia nilivyoona kupitia Televishen ya Taifa ukishuka kutoka kwenye Air Force One, tatu nikafurahishwa vile ulivyochangamka ukiwa pale uwanjani kama haitoshi nikavutiwa vile ukidance pale uwanja wa ndege na kama bado nikapendezwa na uwezo wako wa kujibu maswali ya wanahabari ingawa nilipenda yaendelee.

Mr President nasikitika sijasikia habari ya michezo ikipewa kipaumbele katika ziara yako nilitegemea kusikia katika miradi ambayo serikari yako inafadhiri nchi yetu basi angalau suala la kujenga shule za michezo kwa kasi lingekuwa linagusiwa ,

Mr President ajira imekuwa ni tatizo kubwa katika nchi yetu hasa kwa vijana na labda tulitegemea uwepo wa uwekezaji katika michezo ungesaidia kupunguza tatizo hili ila nalo limekuwa tatizo sugu, sasa kwa mtazamo wangu Capt Mkami Jr nilitegemea itaondoa tatizo hili japo si sana ila angalau michezo uleta watu karibu na uleta furaha na amani.

Mr President pichani nimevutiwa ukiwa na mpira wa mkipasiana na Mr President mwenzio bila shaka kuna chochote mlizungumza kuhusia na hicho mnachokifanya hapo pichani, pia hii picha  kwangu inanipa neno
 
Je Mr President wangu ndugu Jakaya , Uwanja wa taifa,Kocha, na Timu ya taifa vinatosha kutupeleka World Cup mimi nadhani ipo haja ya kuwekeza katika michezo kwa nguvu na kwa mipango hakika tutaweza?

Capt Mkami Jr
source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment