WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, July 5, 2013

Mambo ya kujifunza toka kwa Obama


Obama akiwa na mkewe 


Dar es salaam. Kuna mambo mengi ambayo yanaonekana kama ni funzo kwa Watanzania kutoka kwa Rais wa Marekani, Barack Obama.
Mojawapo ya mambo hayo ni umuhimu wa viongozi kujali wananchi na taifa kwa jumla kama njia ya kusaidia kuharakisha maendeleo.

Sifa za kiongozi bora
Kulingana na wasomi, Cleeton na Mason (1934) uongozi maana yake ni hali ya kuonyesha uwezo wa kushawishi watu, na matokeo ya kiongozi huonekana kwa namna ambavyo anakubalika au hakuliki katika jamii. Kiongozi hupata mafanikio kupitia kushawishi watu hatimaye wafanye kwa hiari yao, siyo kwa kutumia nguvu.

Kitendo cha wingi wa watu waliometanda barabarani katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kumlaki Obama ni ishara nzuri ya kuwa ni kiongozi wa watu.

Ziara yake Afrika
Obama alianza ziara yake Afrika hivi karibuni kwa kuanza kutembelea Senegal, ambako aliisifia kwa kuzingatia demokrasia na kusema kwa hakika inafaa kuigwa na mataifa mengine ya Afrika.

Baadaye akaenda Afrika Kusini, ambako pamoja na mambo mengine alitembelea Kisiwa cha Robben, mahali ambapo Nelson Mandela alifungwa kwa miaka 27.

Aidha baada ya kutoka Afrika kusini, Obama aliingia Tanzania. Aliongea mambo mengi, ikiwemo kusifia uwepo wa amani nchini.

Anaipenda Afrika
Obama anaipenda Afrika, ni bara alilozaliwa baba yake mzazi, Dk Barack Hussein Obama, Sir. Baba yake alikufa katika ajali ya gari Nairobi, ni baada ya kuandamwa na mfumo wa Serikali ya Mzee Jommo Kenyatta, kwa vile tu, baba yake Obama alikuwa anafikiri tofauti na watawala.

Baba yake Obama alikuwa rafiki wa karibu sana wa Tom Mboya aliyeuawa katika mazingira ya kutatanisha. Inaaminika, aliuawa kwa vile alifikiri tofauti na watawala, baba yake Obama inadaiwa alikuwa ana siri juu ya kifo cha Mboya.Obama anazijua vizuri siasa za Afrika.


Serikali isimamie vizuri miradi
Akiwa nchini, Obama aliitaka Serikali ya Tanzania kusimamia vizuri miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ambayo Serikali yake imeingia mikataba na Serikali ya Tanzania.

Obama na uwazi
Akizungumza mbele ya mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete, Rais Obama alisema utamaduni wa kuchelewesha utekelezaji wa miradi haufai kufumbiwa macho kwani unakawiza maendeleo kwa wananchi wenye shida.

“Utakuta mradi unakaa kwa miaka saba au minane bila ya kutekelezwa, jambo hilo hatutaki litokee. Mara mradi unapopangwa na mipango kukamilika, basi utekelezwe haraka iwezekanavyo ili wananchi waone faida zake,” alisisitiza Rais Obama.

Tanzania siyo tu imekuwa ikilaumiwa kwa kuchelewesha utekelezaji wa mikataba, bali hata fedha zinazotengezwa kwa ajili ya shughuli fulani zimekuwa hazipelekwi kwa wakati, kama ambavyo katika bunge lililopita wabunge kadhaa waliwahi kulalamika.

Obama na ndoa yake
Anaonekana ni mwenye kuipenda ndoa na familia yake kutoka usoni na hata matendo yake, tofauti na hali ilivyo kwa ndoa nyingi za viongozi na wanasiasa wa Afrika ambazo baadhi yake ni maigizo, huku kukiwa na kashfa na makahaba kuongezeka Dodoma wakati wa vikao vya Bunge, madai ambayo wanasiasa wamekuwa wakiyakanusha vikali kuwahusisha nao.
Wapo wanasiasa nchini wanadaiwa kuwa na utitiri wa wanawake kila kona, wanaoa kila wanapojisikia, nje wana heshima lakini ndani wananuka kwa uchafu wa ngono za kila aina.

Maisha ya Obama yanatoa funzo na yanaonyesha umuhimu wa wanasiasa kuwa wasafi katika suala la ndoa pia.Obama huwa karibu na familia yake, hucheza na watoto na hata mbwa wake.

Kuna wanasiasa nchini hawana muda na familia zao, bize na anasa, akitoka kazini anaishia baa kunywa na wenza wa nje, sio mumewe au mkewe.

Hii kwa mujibu wa msomi wa masuala ya uongozi, Richard Bass, sio maisha yanayofaa kwa kiongozi.Je, ndio za wanasiasa na viongozi wa Tanzania zikoje? Jibu sahihi wanalo wenyewe.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment