WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, January 23, 2014

Dk. Slaa, Lissu, Mnyika wazindua 'Pamoja Daima'

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Wilbroad Slaa akiwa mkoani Ruvuma jana, kwenye kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilianza Operesheni Pamoja Daima katika maeneo tofauti nchini huku viongozi wake wakitoa kauli mbalimbali.
Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, alihutubia mikutano katika maeneo ya Mbambabay, Mbinga mjini, Peramiho, Namtumbo, Songea mjini akisema chama hicho kimeamua kusambaza fomu nchi nzima na kuwa kimewataka wananchi wote ambao wanahitaji kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura waweke saini zao.

Alisema kuwa suala la kuboresha daftari la wapiga kura si kitu cha mzaha na chama hicho kitasimamia kuhakikisha kila mwananchi anayestahili, anapata haki ya kupiga kura kabla ya kura ya maoni ya kuamua katiba mpya.

Akizungumza katika maeneo ya Mbambabay, Mbinga mjini, Peramiho, Namtumbo na Songea mjini, Dk. Slaa alisema kuwa katika fomu hizo ambazo zitasambazwa na chama hicho nchi nzima, watahitaji wananchi wote ambao kwa namna moja ama nyingine, mfano wamepoteza vitambulisho vyao, wamehama au wametimiza umri lakini hawajaandikishwa, waandike majina yao.

“Tunataka tujue idadi hasa ya wananchi ambao hadi sasa kutokana tu na Serikali ya CCM kuvunja sheria kwa makusudi hivyo daftari la wapiga kura halijaboreshwa tangu mwaka 2010. Katika fomu hizo wananchi wataandika majina yao na taarifa zao zingine kama mahali walipo. Zitagawwiwa kwa wananchi nchi nzima tukianzia na kwenye mikutano ya operesheni hii,” alisema.

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Issa Mohamed na Mkurugenzi wa Habari na uenezi, John Mnyika ilihutubia mikutano (Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini).

Katika mkutano wa Ndala, Nzega mkoani Tabora wananchi walitoa sauti za kulalamikia ongezeko la bei ya umeme huku wakilaani madhara ya Operesheni Tokomeza Ujangili, ambapo pia walitaka kujua kuhusu matumizi ya rasilimali za taifa na kauli za viongozi kufunga mijadala juu ya suala la gesi.

Akijibu swali hilo, John Mnyika ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alisema: “Rais Kikwete hawezi kufunga mjadala wa rasilimali za nchi, ikiwamo rasilimali mkakati na nyeti ya gesi. Mjadala kuhusu wananchi kunufaika na rasilimali uhamie kwa wananchi wenyewe, si kufungwa na viongozi wa serikali. Chadema sasa, kupitia operesheni hii kwa mara nyingine tena inaleta kwenu mjadala huu ili sote tuhoji namna rasilimali za taifa zinavyosimamiwa na kutumika.”

Mnyika aliwaambia wananchi wa Nzega wakumbuke jinsi wakazi wa Lusu jirani na uliokuwa mgodi wa dhahabu wa Nzega Golden Pride Mine Ltd, walivyohamishwa kwa mitutu ya bunduki miaka ya 90.

Mnyika aliongeza kusema kuwa hata wakati huo zilitolewa kauli kama za hivi sasa kuhusu gesi lakini hadi leo wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya migodi na Watanzania wengine kwa ujumla hawaoni manufaa ya wazi kuhusu rasilimali zao.

Mikutano mingine ilihutubiwa na Mhadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni, Lissu na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Vijana (Bavicha), John Heche, katika maeneo ya Lushoto , Korogwe, Muheza na Tanga mjini.

Lissu aliwataka Watanzania, hususan wanachama wa chama hicho kutopoteza muda kujadili suala la baadhi ya wanachama waliopatikana na makosa ya usaliti na utovu wa maadili ndani ya chama hicho, kisha kuchukuliwa hatua bali wajikite kukiimarisha chama hicho kila mahali na kujadili masuala yanayowahusu wananchi.

Lissu alisema taifa linakabiliwa na masuala mengi ambayo yanahitaji umakini wa kila mwanachama wa chama hicho akitolea mfano wa kujadili maudhui ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, ili taifa lipate katiba mpya na bora.

Heche alisema vita na kuutokomeza ufisadi ambao unaendelea kulitafuna taifa akidai unalelewa na Serikali ya CCM, wananchi hawatapata matumaini na maendeleo wanayoyahitaji. 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment