WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, January 24, 2014

Dk. Bilal awataka Wazanzibar kutofarakana

Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi.
Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mohammed Gharib Bilali amewataka Wazanzibari kudumisha umoja, mshikamano na amani ya nchi badala ya kuvurugana kwa misingi ya tofauti za itikadi za kisiasa.
Alitoa rai hiyo wakati akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM wakati akifunguwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar jana.

Alisema kuna kila sababu ya kuienzi hali ya amani na usalama iliyopo ambayo imedumishwa tangu mwaka 1964 na Rais wa kwanza wa visiwa hivyo, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Alisema CCM ndicho kilichodumisha hali ya amani na usalama na mshikamano wa Wazanzibar, hivyo chama hicho hakiko tayari kuona hali ya amani na usalama inatoweka.

“Ukikiona chema kilinde na ukitunze hivyo tutaendelea kuitunza amani yetu” alisisitiza Dk. Bilali. Aidha, Dk. Bilal alisema CCM kitaendelea na msimamo wake wa kutaka mfumo wa muungano wa serikali mbili uendelee kwani ndiyo uliodumisha hali ya amani na usalama na umoja wa kindugu uliopo.

Akimnadi mgombea wa uwakilishi kupitia chama hicho, Dk Bilali aliwataka wananchi wa jimbo hilo siku ya uchaguzi Februari 2 mwaka huu kutofanya makosa ya kuwapa kura wagombea wa vyama vingine bali kumpa kura mgombea huyo wa CCM ili aweza kuleta maenddeleo jimboni humo.

Nae mgombea huyo, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ili aweze kusaidiana nao kuleta mabadiliko ya maendeleo jimboni humo, huku akiwaahidi vijana kuwatafutia njia mbadala za kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira.

Katika mkutano huo wagombea 12 ambao walijitokeza kuwania nafasi hiyo ndani ya chama cha mapinduzi lakini hawakuibuka na ushindi kutokana na kura chache walizopigiwa kutoka ngazi ya tawi, shina, wilaya hadi halmashauri kuu ya chama hicho, waliahidi mbele ya mkutano huo kuwa hawatakuwa na makundi na kutaka wananchi kumpa kura za ndiyo mgombea huyo wa CCM.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment