WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 17, 2014

PICHA ZAIDI ZA MASHAMBULIZI MAPYA KENYA....WATU 48 WAUWAWA..AL-SHABAAB WAHUSISWA


WATU 48 wameripotiwa kuuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo cha mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya jana usiku.Kituo cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka leo  asubuhi .Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kutuo hicho cha polisi baada ya kushambulia.

  
Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.
 
Wananchi walikimbilia katika nyumba zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia”wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.
  
Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo



   

No comments:

Post a Comment