WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, June 8, 2014

IBADA YA KIISLAMU KUFANYIKA VATICAN

IBADA YA KIISLAMU KUFANYIKA VATICAN ( MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI ) KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA

Kwa mara ya kwanza katika historia, sala na mafundisho kutoka kwenye Quran yatasikika Vatican Jumapili, ambako ni makao makuu ya kanisa katoliki duniani.

Uamuzi huo umefanywa na Papa Francis ikiwa ni hatua ya kutengeneza mazingira ya amani kati ya waisrael na wapalestina.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani aliwaalika rais, Shimon Peres na rais wa Palestina Mahmoud Abbas kwenda Vatican pale alipozitembelea Palestina na Israel hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Times of Israel, marais wote wawili wamekubali mualiko huo. Msemaji wa ikulu ya Israel ameeleza kuwa watasindikizwa na viongozi wa dini za kikristo na kiislam.

Kwa mujibu wa Associated Press, Papa Francis amesema kuwa kutakuwa na maombi ya jioni jumapili hiyo pale watakapokutana na kwamba yatalenga kusaidia amani kati ya matakwa ya wapalestina na waisrael katika nyanja zote.

source: matukiotz.com

No comments:

Post a Comment