WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, June 2, 2014

MUTHARIKA AAPISHWA URAIS MALAWI

mth_f9ee5.jpgmth1_81187.jpg
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Progressive nchini Malawi, Peter Mutharika, ameapishwa leo kama rais wa nchi hiyo. Bw Mutharika mwenye umri wa miaka 74 alisema katika hotuba fupi kuwa kazi yake kubwa itakuwa kuwaunganisha wamalawi baada ya mvutano wa muda mrefu katika maswala ya uchaguzi.(Martha Magessa)Ametoa wito kwa washindani wake kuungana naye katika kujenga taifa. Maafisa uchaguzi Ijumaa walimtangaza Mutharika kama mshindi wa uchaguzi wa wiki iliyopita uliokuwa na utata na kumshinda rais aliyekuwa madarakani Joyce Banda.

Tume ya uchaguzi ya Malawi ilitangaza matokeo hayo Blantyre, saa kadha baada ya waandamanaji waliokuwa wakidai hesabu mpya ya kura kupambana na polisi katika mji wa Mangochi – kusini mwa nchi. Inaripotiwa kuwa mtu mmoja alifariki katika ghasia hizo.

Hesabu ya mwisho inayonyesha kuwa Bw Muthariki alipata kiasi cha asilimia 36 ya kura, na chama cha Malawi Congress cha Lazrous Chakwera kilipata asilimia 29. Rais Banda alimaliza na asilimia 20 tu ya kura. Bw Mutharika ni kaka wa rais wa zamani marehenu Bingu wa Mutharika.
CHANZO:VOA

No comments:

Post a Comment