WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, January 10, 2013

HOJA YA JK KUHUSU UBUNGE WA KAFUMU YAIBUA MAPYA


nz8 2a457
KITENDO cha Rais Jakaya Kikwete kuhoji hukumu iliyomwengua Dk Dalaly Peter Kafumu kuwa Mbunge wa Igunga, kimewakera baadhi ya wanasheria nchini ambao wameeleza kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola. Akizindua Daraja la Mbutu mkoani Tabora, Januari 7, mwaka huu, Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, alihoji uamuzi uliomwengua katika nafasi ya ubunge Dk Kafumu kwa kigezo cha kufanya kampeni kwa kutumia ujenzi wa daraja hilo.


Rais Kikwete alihoji mantiki ya uamuzi huo wakati ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mambo yaliyopo kwenye Ilani ya CCM ya 2010 – 2015.

“Mwaka 2010 katika Uchaguzi Mkuu nilifika hapa kumnadi aliyekuwa mbunge wa jimbo hili, Rostam Aziz na ujenzi wa Daraja la Mbutu ni moja ya mambo yaliyopo kwenye ilani yetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Katika uchaguzi mdogo baada ya kujiuzulu Rostam, CCM iliendelea kunadi ilani yake ya kujenga daraja hilo kwa kuwa lilikuwa halijakamilika baada ya mbunge wake kujiondoa.”

Akizungumzia kauli hiyo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society (TLS), Francis Stola alisema hukumu hiyo ilikuwa sahihi kwani ni makosa kwa kiongozi wa Serikali kutumia jukwaa la kampeni za kisiasa kuzungumzia masuala yanayohusu utendaji wa Serikali akisema kufanya hivyo kunaweza kutoa ushawishi kwa wapigakura na kuvuruga mwenendo wa uchaguzi.

“Kiongozi wa Serikali haruhusiwi kutoa kauli ambayo kwa namna moja au nyingine, inaweza kutibua mwenendo wa uchaguzi au kufanya wapigakura wasiwe na uamuzi huru,” alisema Stola na kusisitiza kuwa katika nchi inayosimamia misingi ya demokrasia na utawala wa kisheria, viongozi wa Serikali hawapaswi kutumia rasilimali za umma kwa ajili ya kupata mtaji wa kisiasa.”

“Ndiyo maana pia hairuhusiwi wakati wa kampeni kumwona kiongozi wa Serikali akitumia rasilimali za umma kama vile kutumia magari ya Serikali kuendesha kampeni za kisiasa,” alisema Stola.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema suala hilo linahitaji utafiti na siyo la kulizungumzia juujuu.

“Hilo ni suala la kiutafiti bwana. Fanya utafiti wako halafu uje tujadiliane.”
Wakili wa kujitegemea, Mpale Mpoki alisema Serikali haipaswi kutoa ahadi za kufanya jambo fulani wakati wa kampeni kwa kuwa hilo ni jukumu ambalo lilipaswa kufanywa bila kusubiri uchaguzi.

“Hata mgombea mwenyewe awe wa chama tawala au chama kisichokuwa madarakani, hapaswi kutoa ahadi kama zile za kujenga barabara, daraja au kufanya jambo lolote.”

“Kwa mtazamo wangu ni makosa mbunge akienda kwenye kampeni kujitangaza kwamba yeye mwenyewe akiwa mgombea atajenga daraja. Kujenga daraja au barabara si kazi ya mbunge, akifanya hivyo atakuwa akiwarubuni wananchi na inakuwa mbaya zaidi Serikali inapofanya hivyo.”

MWANANCHI

No comments:

Post a Comment