MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mkurugenzi wa Cloud’s Media Group, Ruge Mutahaba, wachezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Khalid Abeid, Talib Hilal, Zamoyoni Mogela, Yusufu Macho na Shaban Baraza wameteuliwa katika kamati mbalimbali za klabu hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema majina hayo yamo katika kamati zake tatu mpya, ambazo zimeundwa baada ya zile za awali kuvunjwa.
Kamwaga alisema lengo ni kuiboresha klabu na pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa, ambayo Simba inashiriki mwaka huu. Alisema uteuzi huo wa wajumbe unaanza mara moja na wenyeviti wa kamati hizo wamepewa nguvu ya kuitisha vikao vya kamati zao mapema iwezekanavyo. Kamati ya Fedha, Mwenyekiti atakuwa Geofrey Nyange ‘Kaburu’, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Rahma Al Khaloos ndiyo Makamu wa kamati hiyo na wajumbe katika kamati hiyo ya fedha ni Kabwe, Francis Waya, Ruge Mutahaba na Juma Nkamia.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Swedy Nkwabi, ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, huku Makamu wake akiwa mjumbe mwingine wa Kamati ya Utendaji, Said Pamba na wajumbe ni Seleman Zeddy, Jerry Yambi, Idd Kajuna, Chaurembo, Gerard Lukumay na Habbi Nassa.
Wengine ni Bundala Kabulwa, Said Rubeya, Charles Hamkah, Abdulfatah Salu, Hatibu Mwinyi, Abdul Mshangama, Humphrey Zebedayo, Majaliwa Mbasaa, Suleiman Zakazaka na Mohamed Mbena.
Kamati ya Ufundi ipo chini ya Damian Manembe, makamu wake ni Ibrahim Masoud, wakati wajumbe ni Crescencius Magori, Khalid Abeid, Said Tully,Mogela, John William, Yusuf Macho, Dk. Kategile, Jeff Lea, Bira John na Shaban Baraza.
Kamati ya Programu Maalumu za Vijana itakuwa chini ya Ibrahim Masoud, Makamu wake atakuwa Ruge Mutahaba, wakati wajumbe katika kamati hizo ni Joseph Itang’are. Wilfred Kidau, Mohamed Abdallah, Said Tully, Canisius Masombola, Hamis Mrisho, Damas Ndumbaro na Talib Hilal.
Pia, Kamwaga alisema timu yao inarejea leo kutoka Oman saa 10 jioni, na itaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya African Lyon Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
source: jambo leo
No comments:
Post a Comment