NA MWANDISHI WETU
Goli lililofungwa na mshambuliaji Mrisho Ngassa wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na kuipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Zambia (Chipolopolo) kwenye Uwanja wa Taifa Desemba 22, 2012 limeiinua Tanzania na kuwaporomosha mabingwa hao wa Afrika katika orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa jana Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Taarifa iliyotolewa ja na FIFA kuhusiana na viwango vya mwezi huu inaonesha kuwa Zambia imeporomoka kwa nafasi tano na kushika nafasi ya tano barani Afrika na ya 39 duniani huku Tanzania ikikwea kwa nafasi sita na kushika nafasi ya 124 duniani na ya 36 barani Afrika.
Nafasi ya kwanza barani Afrika inashikiliwa na Ivory Coast ambao wanafuatiwa na Algeria, Mali, Ghana, Zambia, Libya, Gabon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria na Tunisia katika kukamilisha 'top 10' barani.
Uganda ambayo imepanda kwa nafasi tatu duniani, inaongoza katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwa katika nafasi ya 21 Afrika na 81 duniani, ikifuatwa na Burundi (29 barani), Tanzania, Kenya (38) na Rwanda (40).
Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) unaongozwa na Uganda, Sudan, Burundi, Ethiopia, Tanzania, Kenya, Rwanda, Ertrea, Sudani Kusini, Somalia na Djibouti.
Nafasi 10 za juu duniani zinashikiliwa na Hispania, Ujerumani, Argentina, Italia, Colombia, England , Ureno, Uholanzi, Urusi na Croatia.
Mabingwa wa Afrika, Zambia watakuwa na nafasi ya kukwea tena katika viwango vya ubora wa soka mwezi ujao wakati watakapokuwa wakitetea ubingwa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazoanza kesho nchini Afrika Kusini.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment