Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake stesheni ya Saranda, mkoani Singida,jana mchana. Kinana na msafara wake wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai.
Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake, wakikaribishwa na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma baada ya treni kutoka Dar es Salaam, kuwasili leo asubuhi mjini Kigoma, Wanaoshuka ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma kwenye stesheni ya Kigoma, alipaowasili kwenye stesheni hiyo na ujumbe wake akitokea jijini Dar es Salaam. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Nape akishiriki kupiga ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Kinana akisalimiana na wananchi kwenye stesheni ya Kazuramimba leo saa 12, asubuhi. ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru dereva wa treni Kambi Ali, baada ya treni ya abiria aliyoendesha akiwemo Kinana na ujumbe wake kuwasili mjini Kigoma leo asubuhi. Wengine Wapili kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro na Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma kwenye stesheni ya Kigoma, alipaowasili kwenye stesheni hiyo na ujumbe wake akitokea jijini Dar es Salaam. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Nape akishiriki kupiga ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) wakisindikizwa baada ya kushuka kwenye treni mjini Kigoma, ambako waliwasili leo wasubuhi wakitoka jijini Dar es Salaam.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimfurahia mtoto Ali Saidi mwenye umri wa miezi minane, ambaye ni mtoto wa mmoja wa abiria aliowakuta kwenye Stesheni ya Kigoma, msafara wa Kinana ulipowasili leo kwa treni.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Abiria kutoka Tabora kwenda Kigoma wakiwa katika behewa leo.
Kinamama wa Uvinza, wakipeleka kuuza chumvi kwa abiria, treni ilipofika kwenye stesheni ya eneo hilo la Uvinza leo ikitoka Dar es salaam kwenda Kigoma
SOURCE HAKI NGOWI
No comments:
Post a Comment