WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, January 16, 2013

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI LEO



Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya picha zote na Tume ya Katiba.

Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.

source lukwangule blog

No comments:

Post a Comment