WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, January 15, 2013

Jeshi la Polisi linahitaji mapinduzi makubwa



Daniel Mjema 
NI kwamba Jeshi la Polisi nchini linahitaji mapinduzi makubwa ili kulirejeshea imani kwa wananchi na hatimaye kufanikisha mkakati wake wa ulinzi shirikishi.

Matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya vyama vya siasa, ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, matumizi holela ya silaha za moto, kushiriki uporaji, ujangili na matendo mengine mabaya kumechangia kuongezeka kwa chuki kati ya polisi na wananchi.

Miaka ya nyuma hatukuwahi kushuhudia matukio ya kutisha ya wananchi kuua polisi hadharani, lakini sasa polisi wetu wanauawa na raia. Hii si hali ya kawaida hata kidogo, na haitakiwi kuachwa iendelee kwani inaweza kuleta madhara makubwa.


Katika makala yangu moja niliwahi kusema hapa kwamba ‘tusiwakomaze wananchi wetu kwa risasi na mabomu’. Niliyasema hayo nikitazama namna uhusiano kati ya polisi na raia ulivyokuwa unazidi kuyumba. Jeshi la Polisi linalalamikiwa kutumika zaidi kisiasa na kutofanya kazi kwa weledi. Kanuni zinakataza polisi kushabikia chama chochote cha siasa lakini matendo yao ni kinyume na dhana hiyo.

Ipo mifano mingi tu kuthibitisha kuwa kwa baadhi ya mazingira, polisi wetu wamekuwa wakidaiwa kutekeleza wajibu wao kwa kuipendelea CCM ama kwa kujua au kwa kushawishiwa na ‘wenye nchi’ kufanya hivyo.

Mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi ni matokeo ya polisi kufanya kazi zao kwa double standard (upendeleo) na kuvikandamiza vyama vya upinzani.

Polisi walipopiga marufuku mikutano ya Chadema kwa kisingizio cha Sensa papo hapo kuruhusu mikutano ya ndani ya CCM na ile ya kampeni Zanzibar hakika hapa jeshi letu lilionyesha upungufu mkubwa wa weledi.

Lakini mbali na tukio hilo la Iringa, bado polisi wamekuwa wakikataa kutoa vibali vya baadhi ya mikutano ya vyama vya upinzani kwa ‘kupiga ramli’ eti intelejensia inasema kutatokea vurugu.
Wakati yote haya yakitokea hakuna mahali tumesikia mikutano ya hadhara ya CCM imezuiwa. Tena wenzao CCM wanaomba ‘vibali’ kwa muda mfupi na kuruhusiwa. Hapa tuna tatizo la msingi.

Siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu, lakini upendeleo huu unaofanywa na Jeshi la Polisi hakika usipodhibitiwa ndio utakuwa chanzo cha machafuko nchini. Tunahitaji mapinduzi makubwa.

Tukiachia medani hizo za kisiasa, lakini hata huko uraiani kwenyewe, uhusiano kati ya polisi na raia si mzuri na hata ile dhana ya Polisi Jamii inaonekana tu kama kiini macho. Mauaji ya polisi huko Mara na maeneo mengine ni kielelezo dhahiri kuwa hali ya uhusiano kati ya raia na polisi si mzuri. Raia wanapowavamia polisi na kuwaua si jambo la kawaida hata kidogo. Halikubaliki. Na namna pekee ya kuondokana nalo moja kwa moja ni kutenda haki, na haki ikaonekana inatendeka.

Polisi wenyewe ndio wamewakomaza Watanzania kwa mabomu na risasi zao, athari zake ndio zimeanza kujitokeza. Ni zimwi walilolitengeneza wenyewe sasa limeanza kunywa damu yao.Miaka ya nyuma ulikuwa ukimuona polisi hata kama wewe si mhalifu unatetemeka. Watu walikuwa wanaheshimu kofia, leo wananchi wamefikia hatua wanapigana na polisi.

Wananchi wamekomazwa na kubambikiwa kesi. Wananchi wamechoshwa na upelelezi dhaifu unaosababisha wahalifu wa kweli kuachiwa huru na wasio na hatia kulundikana magerezani.

Tunahitaji mapinduzi makubwa ya kiutendaji katika jeshi hili. Tunataka polisi wa upelelezi wasigeuke kuwa mabingwa wa kuwafundisha watuhumiwa namna ya kuandika maelezo ya kuwatoa. Tunataka vituo vya polisi visigeuzwe kama maduka kwamba mtuhumiwa kuingia ni bure lakini kutoka ni pesa. Tunataka dhamana iwe ni haki ya mtuhumiwa na isishinikizwe na hongo au rushwa.

Katika mapinduzi hayo, tunataka maofisa wetu wa polisi wasijiingize kwenye mitandao ya kihalifu na kusubiri migawo baada ya uhalifu kufanyika. Ndio! Wapo wanaoshirikiana na makundi ya kihalifu.

 Mapinduzi haya yasiishie tu kuangalia mabaya ya polisi wetu. Tutazame makazi yao. Haiwezekani tuadhimishe miaka 51 ya Uhuru huku Polisi wakiishi nyumba zisizokuwa na hadhi waka kulinda na kuhifadhi utu wao.

Mwananchi

No comments:

Post a Comment