WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, January 30, 2013

Mamilioni ya Okwi Simba bado saa 48


NA SOMOE NG`ITU

mshambuliaji wa Simba Mganda Emmanuel Okwi

Mabingwa wa Soka wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wakati wowote kuanzia leo na kesho wanatarajia kuanza kupokea awamu ya kwanza ya fedha za usajili za aliyekuwa mshambuliaji wao, Mganda Emmanuel Okwi ambaye ameuzwa katika timu ya Etoile du Sahel inayoshiriki Ligi Kuu ya Tunisia.

Simba imemuuza Okwi kwa dau la dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 475) na wakati wowote klabu hiyo itapokea kiasi cha dola za Marekani 150,000 (Sh. milioni 237.5) kama walivyokubaliana.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange 'Kaburu', alisema kuwa makubaliano yao na klabu ya Etoile du Sahel yalikuwa ni kuwalipa kwa awamu mbili na kwamba watamalizia fedha zote mwishoni mwa mwezi ujao.

Kaburu alisema kwamba baada ya kupatikana kwa fedha hizo, Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo itakutana na kupanga mikakati mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha timu inashinda mechi zake za ligi kabla ya kuanza maandalizi ya mechi zao za Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

"Makubaliano ni kulipwa mara mbili na awamu ya kwanza ni leo (jana) Januari 28 na Februari 28, lakini kwa kuwa zinatumwa kutoka nje ya nchi, tunaamini kuwa itachukua siku mbili (saa 48) ili nasi tuweze kuzipata nchini," alisema Kaburu.

Kaburu aliongeza kuwa fedha zote zinazoingia katika klabu hiyo na kutumika, maelezo yake yanawekwa katika taarifa za fedha hivyo na hivyo wanachama na mashabiki wasiwe na hofu yoyote.

Habari ambazo zimepatikana kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa fedha ambazo Simba ilizipata kwa kumuuza mshambuliaji Mbwana Samatta kwa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ziliingia katika akaunti ya mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo na si akaunti ya klabu..

Samatta aliyetokea African Lyon ya jijini Dar es Salaam, aliuzwa kwa dola za Marekani 150,000.
Mchezaji mwingine wa klabu hiyo aliyeuzwa kwa kiasi kikubwa cha fedha ni Mganda, Patrick Ochan ambaye alisajiliwa kwa pamoja na Samatta katika klabu ya Mazembe.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment