Katibu Mkuu wa
CCM,Abdulrahman Kinana mwananchi
Na n Happy Lazaro, Arusha
KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za
kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu ya dini
na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa kuliombea taifa , ili
wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere.
Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho ya siku ya
kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la KhojaShia Ithna
Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jumuiya hiyo
jijini hapa , ambapo watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa madhehemu pamoja na
viongozi wa chama na Serikali walihudhuria.
Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa viongozi wa dini na
taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na
kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za haraka kwa mtu ama kikundi
chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjivu wa amani.
Alisema pamoja na changamoto zinazojitokeza hivi sasa kwa baadhi
ya dini kukashifu dini zingine ,Serikali ipo macho kuhakikisha kwamba
inadhibiti hali yoyote ya ukiukwaji wa maadili ya kidini nakusisitiza kwamba
dini zote nchini ziendeshe shughuli zake kwa kuheshimiana.
‘’Usidharau imani ama itikadi ya mtu mwingine lazima dini
ziendeshwe kwa maadili na sio kiholela,kama hupendi kubaguliwa kwa dini usiwe
mwepesi kubagua dini ya mwingine’’alisema Kinana. Alisisitiza kwa kuyataka
madhehebu ya dini kuiga mfano wa kujenga ushirikiano na mshikamano katika
kutangaza neno la Mungu na kuepuka mifarakano inayoweza kuwagawa watanzania
kiimani,na kuwataka viongozi wa dini kuwa wa kwanza kukemea hali hiyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia, Gulam Hussen
alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuendelea kukumbuka mazuri yote
aliyokuwa akiyafanya Mtume Muhammad kwa lengo la kukumbushana na kuyaenzi.
Alisema maadhimisho yao yaliyotambulika kwa jina la ‘Hussein
Day’yanalenga kujenga undugu ,kufahamiana na kupinga ufisadi unaolinyemelea
taifa kwa baadhi ya viongozi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali.
Aliitaka jamii ijifunze kuishi maisha ya kitume huku ikijali
haki na usawa duniani na kuepusha migogoro ya kidini ambayo haina tija
,aliwataka waislamu wajifunze kuishi kwa upendo.Naye mkuu wa wilaya ya Monduli,
Jowika Kasunga aliyekuwa amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo,alisema serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika
kuboresha huduma za maendeleo kwa wananchi.
Alizitaka dini zote hapa nchini ziendelee kudumisha amani na
kudai kuwa iwapo amani itaachwa ichezewe ,gharama za kuirudisha ni kubwa sana
hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na vifo .
Alisema kuwa tayari serikali imepata taarifa kuwa wapo watu
ambao wamekuwa wakijipenyeza kwa ajili ya kuvuruga amani kwa kutumia mgongo wa
dini ,na kusema kuwa imejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi ana uhuru wa
kuabudu popote bila kubughudhiwa na kwamba itakabiliana na wenye nia ya kuleta
chokochoko za kidini.
chanzo Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment