WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, January 3, 2013

SIMBA YAANZA VIZURI MAPINDUZI CUP

Simba, Jamhuri zakata utepe Mapinduzi
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad akisalimiana na kiungo wa Simba SC, Kiggi Makassy, nyuma yake ni Haruna Moshi na Paul Ngalema kabla ya mchezo wa jana wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Simba ilishinda 4-2.
Mwenyekiti wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu akisalimiana na mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad akipiga penalti jana katika ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi kabla ya mechi kati ya Simba SC na Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Simba ilishinda 4-2.
Kikosi chs Simba SC jana
Mchezaji wa Jamhuri akigombea mpira na mchezaji wa Simba
kwa picha zaidi bofya read more
Mwinyi Kazimoto akimtoka mchezaji wa Jamhuri
Miraj Adam akipanda kusaidia mashambulizi
Shomary Kapombe akipambana na mchezaji wa Jamhuri
Mchezaji wa Jamhuri akipambana na wachezaji wa Simba
KIpa Jaffar Said wa Jamhuri akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba SC, Felix Sunzu huku akilindwa na beki wake
Kizazaa langoni mwa Jamhuri
Kiungo wa Simba, Haruna Chanongo akiifungia Simba bao la kwanza kwa kichwa 
Chanongo akimshukuru Kiggi Makassy kwa kupiga kona nzuri aliyoiunganisha nyavuni kwa kichwa (hapo juu)
Simba SC wakishangilia ushindi wao jana.
 (picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog)

PAZIA la michuano ya Kombe la Mapinduzi,  linafunguliwa leo kwa michezo miwili kwa Simba kuivaa Jamhuri ya Pemba, huku Tusker ya Kenya wakipepetana na Bandari mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri ya mchezo, lakini amesisitiza mashindano hayo yatasaidia kujenga timu imara itakayoiwakilisha Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Nafikiri mashindano haya yamekuja wakati mwafaka.
Pia, tumepata kocha mpya Mfaransa Patrick Liewig.
Ni wakati wetu sasa kushirikiana naye kujenga timu na kufanya makubwa katika Ligi ya Mabingwa.”
“Nadhani mashindano haya tutayatumia zaidi kupata picha halisi ya kikosi chetu. Pia, kutambua uwezo wa kila mchezaji, kiuchezaji,” alisema Julio.
Hata hivyo, kocha huyo ametamba kuwa Wekundu hao wana nafasi kubwa kutwaa kombe hilo, kulingana na ubora wachezaji wanaounda kikosi cha Simba kwa sasa.
Naye, kocha wa Tusker ya Kenya, Robert Matano amesema baada ya kuzifunga Simba na Yanga katika mechi za kirafiki, anafikiri timu yake ina nafasi kubwa kulitwaa kombe hilo kwenye nchi ya Tanzania.
“Nafikiri kuzifunga Simba na Yanga, timu yangu ni nzuri. Sizifahamu vizuri timu nyingine. Lakini naamini tutafanya vizuri na hata kurejea na kombe nchini Kenya.” alisema Matano.
Bingwa watetezi, Azam FC itashuka dimbani kesho usiku kupepetana na Coastal Union huku ukitanguliwa na mchezo kati ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na Miembeni ya Zanzibar.
Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanaifunga Coastal Union kwenye mchezo huo wa ili kulitetea taji lao kwa mara nyingine.
“Hali ya timu kwa jumla ni nzuri. Kila mchezaji ana hari kuhakikisha timu inafanya vizuri na kutetea taji kwa mara nyingine.”
Kocha huyo alisema; “Kila mchezaji ameahidi kucheza kwa kujituma ikiwa ni lengo la timu yake kufanya vizuri na kutetea ubingwa huo.”
“Ni jambo zuri kwangu nikiwa kama mwalimu wa timu kusikia maneno hayo kutoka kwa wachezaji wangu.
Nafikiri ni hatua moja ya mafanikio yetu katika mashindano hayo.” aliongeza.Naye, kocha wa Coastal Union, Hemed Morocco alisema anafikiri mchezo huo utakuwa mgumu na ushindani hivyo hawezi kusema kuwa timu yake itaibuka mshindi isipokuwa dakika 90 ndizo zitakazoamua.
“Nafikiri tumejianda vya kutosha. Tunachosubiri muda ufike tuweze kuwathibitishia mashabiki tulichokuwa tukikifanya kwa wakati wote.” alisema kocha huyo.
Mabingwa hao wamepangwa kundi B pamoja na timu za Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union ya Tanga na Miembeni ya visiwani Zanzibar.
Simba imetupwa kundi A sambamba na mabingwa wa Kenya Tusker FC, Jamhuri ya Pemba na Bandari  ya Zanzibar.
Bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha sh10 milioni wakati makamu wake akiondoka na sh 5 milioni.
Habari na Mwananchi


No comments:

Post a Comment