WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, January 7, 2013

JK AFUNIKA IGUNGA LEO


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wakazi wa Igunga.
Rais Jakaay Mrisho Kikwete akihutumia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Maelfu ya wakazi wa Igunga wakimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa mji huo watapata maji safi
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akijiunga na bendi ya Msondo Ngoma kutumbuiza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Mbutu la Igunga


Wananchi wakivuka katika sehemu itayojengwa darala la kisasa la Mbutu la Igunga ambao ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la miundombinu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10 ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo
Rais Kikwete akiangalia michoro ya Daraja litakalojengwa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake inakaribia kukamilisha ujenzi wa madaraja yote 10 yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na ambayo yanagharimu mabilioni ya fedha.


Rais Kikwete amesema kuwa kati ya madaraja hayo ambayo thamani yake inakaribia sh. bilioni 415, madaraja mawili tayari ujenzi wake umekamilika. Madaraja hayo ni lile la Ruhekei lililoko Wilaya ya Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma na Daraja la Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro.


Rais Kikwete amesema kuwa madaraja mengine saba yanaendelea kujengwa, ikiwa ni  pamoja na Daraja la Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam linalogharimu sh bilioni 214.6, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Mkoa wa Kigoma unaogharimu sh bilioni 90.185, Daraja la Kilombero, Mkoa wa Morogoro linalogharimu sh bilioni 53.214 na Daraja la Rusumo, Mkoa wa Kagera linalogharimu sh bilioni 31.7.


Madaraja mengine yanayoendelea kujengwa ni Daraja la Sibiti, Singida,  linalogharimu sh bilioni 17.5, Daraja la Nangoo, Mkoa wa Mtwara linalogharimu sh bilioni 4.29 na Daraja la Maligisu, Mwanza, linalogharimu sh bilioni 2.51.


Amesema Rais Kikwete: “Madaraja niliyotaja ujenzi wake ukikamilika, tutakuwa tumetimiza ahadi yetu ya kujenga madaraja yote yaliyotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 isipokuwa Daraja la Ruhuhu ambalo maandalizi yake ya ujenzi yanaendelea.”


Rais Kikwete alikuwa anazungumza wakati anaweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mbutu, Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora katika sherehe ya kufanya iliyofanyika  Jumatatu, Januari 7, 2013.


Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya madaraja yanayojengwa sasa na Serikali yalipangwa kujengwa katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo mwaka 1968 lakini kwa bahati mabaya hayakuweza kujengwa. Madaraja hayo ni Daraja la Kigamboni, Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara, Daraja la Rufiji, Daraja la Kilombero, Mkoa wa Morogoro na Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi.


Awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu ilijenga Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara, Awamu na pili ikafanya maandalizi na Awamu ya tatu ikajenga Daraja la Rufiji na Awamu ya sasa inajega madaraja matatu yaliyobakia – Kilombero, Kigamboni na Kikwete.”


Daraja la Mbutu lina urefu wa kilomita tatu, na linajengwa katika Bonde la Mbutu na litaunganisha mikoa ya Tabora, Singida, Simiyu na Shinyanga.

Daraja hilo litakuwa na daraja moja kubwa la mita 60 na madaraja mengine madogo saba na hivyo kufanya urefu wa daraja lote kuwa na mita 165. Mpaka sasa asilimia 45 ya ujenzi wa daraja hili lenye thamani ya sh bilioni 11.28 umekamilika na inakadiriwa kuwa litakuwa tayari ifikapo Novemba mwaka huu.


Mwisho. 


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment