WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, September 25, 2014

BALOZI SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA MTANZANIA .

PIX_1[1]
PIX_2.[1]
PIX_3.[1]
PIX_4.[1]
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014.
PIX_5.[1]
PIX_6.[1]
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kukanusha taarifa zilizoandikwa na Gazeti hilo.
PIX_7.[1]
PIX_8.[1]
PIX_9.[1]
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakifutailia kwa makini taarifa toka Balozi Seif Ali Idd.
BALOZI SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA MTANZANIA KUHUSU KUJIUZULU KWA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
 Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amekanusha madai mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar kujiuzulu’.
 
Akikanush taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa Mhe. Othman alitakiwa ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika Kamati sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.
 
Mhe. Balozi Idd alifafanua kuwa Mjumbe kuchaguliwa katika kamati na kukataa kuhudhuria ni maamuzi yake binafsi na hakuna lazima ya mjumbe kuchaguliwa kuingia katika kamati fulani ikawa ndiyo kifungo licha ya kwamba atakuwa na wajibu wa kuendelea kufanya kazi katika kamati hiyo hadi mwisho.
 
“Sisi kama Serikali tunakanusha suala la sintofahamu iliyoandikwa na gazeti hilo ambayo imedai kwamba Viongozi wa juu wa CCM walikutana kwa dharura na kuazimia kumfukuzwa kazi kwa Mwanasheria huyo kwa kile walichodai amekisaliti Chama”, alisema Balozi Idd.
 
Akizungumzia juu ya uwepo wa hoja 17 ambazo zilitakiwa kuwasilishwa na Mwanasheria Mkuu huyo, aisema kwamba Mwanasheria hiyo tayari alishaziwasilisha n azote ziliingizwa katika Rasimu ya Katiba isipokuwa Hoja Nne ambazo bado zinafanyiwa kazi.
 
Aidha ameongeza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hatakiwi kuwa muumini wa Chama chochote cha siasa na ndiyo maana hata vikao vya chama hatakiwi kuhudhuria, hivyo Mwanasheria huyo wa Serikali si mteule wa chama bali ni mteule wa Mhe. Rais was Zanzibar na ndiyo mwenye maaumuzi ya kumuondoa ama kutomuondoa.
 
Akizungumzia kuhusu tuhuma za kufanyika kwa kikao cha Mawaziri wote wa SMZ wakiongozwa na Dkt. Shein ili kuelezwa taarifa ya Mwanasheria huyo juu ya masuala 17 aliyotaka yaingizwe katika Rasimu ya Katiba alikanusha kuwa, suala hilo sio kweli kwani baadhi ya waandishi wa habari hawafahamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Mfumo wa Umoja wa Kitaifa ambao umeundwa na CCM na CUF.
 
“Kama inavyoeleweka CUF hawamo katika Bunge Maalum la Katiba, sasa itakuwaje washiriki kuchangia masuala ambayo wao kama sehemu ya UKAWA hawakubaliani na kuendelea kwa Bunge hilo?”, alihoji Balozi Idd.
 
Mhe. Balozi Idd amevitaka Vyombo vya habari kuandika habari zenye ukweli na amewataka kupuuzia uvumi unaoenea katika mitandao ya kijamii kuhusu vitisho vitolewavyo na baadhi ya watu wenye nia ya kuwatisha baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwani vyombo vya dola linafahamu juu ya uwepo wa vitisho hivyo na inavifanyia kazi.

source: matukiotz.com

No comments:

Post a Comment