Moja ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamadi baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza leo.


Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.
Habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi umepata ajali ukihusisha magari mawili ya msafara wa kiongozi huyo ambayo jumla yake yalikuwa saba yalipogongana na lori lenye tela. Akizungumza na mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyamagana ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.
source: matukiotz.com
No comments:
Post a Comment