WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, September 5, 2014

ANGALIA PICHA ZAIDI:AJALI MBAYA YATOKEA MUSOMA ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI DUNIA





ANGALIA PICHA ZAIDI AJALI MBAYA ILIYOUWA WATU 25

  
 Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.Watu 25 wamepoteza maisha papo hapo na wengika kujeruhiwa vibaya sana.kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo la ajali.

Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.



 Mabasi hayo yakiwa yamegongana 







Basi la Jumanne lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma.  Endelea kufuatilia 


 Miili ya Abiria waliokufa ikiwekwa vizuri ili kutambuliwa



 Mahututi wakikimbizwa wodini



wanainchi wakiwa kwenye simanzi
Watu wakitambua miili ya marehemu
Basi la Mwanza coach limepata ajali eneo la sabasaba likiwa njiani kuelekea mwanza na kuua watu zaidi ya 30 na majeruhi wengi,Taarifa kamili inakujia punde kaa nasi.Picha na Shomari Binda 
source: matukiotz.com/ 
Maelezo kwa Mujibu wa Father Kidevu blog




1 comment:

  1. Ee MUNGU BABA YETU utunusuru na maafa haya kwetu kwani sasa tunakufa kama kuku wenye kideri!BABA ni wewe tu unaefahamu ukweli wa ajali hizi zinazotokea hapa TZ hususani wakati mgumu huu wa katiba!MUNGU utuokoe mikononi mwa ibilisi!

    ReplyDelete