WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, August 5, 2014

UKAWA RUDINI BUNGENI






Na Happiness Katabazi

MHADHIRI  wangu wa somo la Sheria la Katiba wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), wakili Aghata Leandy  kwa  Miaka miwili mfululizo sasa amekuwa akitufundisha Darasani  somo Hilo na Ilipofika  Topiki ya jinsi ya kutengeneza Katiba.

 Mhadhiri Huyo wa Sheria,  Leandy  alisema   kuna Hatua  Mahsusi  za kupitia Katika Kutengeneza   Katiba  nchi zenye demokrasia na zinazojitawala kwa  Utawala wa Sheria.

Mhadhili Leandy alizitaja  hatua  hizo Kuwa ni kwanza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukusanya maoni ya wananchi (Grass Root Level),  Tume yenyewe kuchambua maoni hayo waliyoyakusunya toka kwa  wananchi  na kisha Kutengeneza  rasimu yake ambayo rasimu hiyo italelekewa Katika Bunge la Katiba.

Tatu ni Bunge la Katiba  (Constitutional Assembly) ambapo bunge la Katiba itaijadili rasimu ya Tume  na kisha bunge hilo kuipigia kula ya ndiyo au hapana Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge na hatua ya mwisho ni kwa Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge la Katiba kupelekwa kwa wananchi ili wananchi nao waweze kupigia kula ya ndiyo au hapana Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge la Katiba( Referundum)

Na Kwa mujibu wa Kifungu Cha 18 Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012 kinaruhusu  Hatua hiyo ya kwanza kufanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Hatua ile ya pili ni rasimu  ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba Katika Bunge Maalum.Kwa hiyo mapendekezo yaliyo Katika rasimu ya Tume ya Warioba siyo maoni ya wananchi ni mapendekezo ya Tume hiyo kwa  Bunge Hilo Maalum. Hivyo kilichobakia ni Bunge kuijadili rasimu  ya Warioba na Kutengeneza Katiba itakayopendekezwa na Bunge Hilo na Kisha wajumbe Hao kuipigia kula ya ndiyo au Hapana Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge Hilo. 

Kwa hiyo kitendo kilichofanywa na UKAWA Cha Kupeleka rasimu ya Warioba kwa wananchi hakikuwa sahihi. Kisheria Rasimu ya Tume inapaswa kupelekwa Katika  Bunge Maalum la Katiba ambalo linaongozwa na Mwenyekiti Samuel Sitta.

Ikumbukwe Kuwa rasimu ya Tume ya Warioba siyo maoni ya wananchi , rasimu ile ni mapendekezo ya Tume ya Warioba, mapendekezo ya Tume siyo mapendekezo ya wananchi kwasababu kisheria wananchi watatoa maoni Yao  kuhusu Katiba wanayoitaka pale tu Wananchi watakapolekewa ile Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum  na kwasasa bado Bunge Maalum bado halijafikia hatua ya Kutengeneza Katiba iliyopendekezwa na Bunge Hivyo naweza Kusema wanachokifanya Ukawa ni kuwavuruga wananchi.

Tuliwasikia baadhi ya wana UKAWA wakidai  CCM inataka kuchakachua rasimu ya Warioba na mchakato mzima , na wengine walidiriki Kusema  kuwa Bunge Hilo Halina mamlaka yoyote yakufanyia marekebisho ama kuongeza wala kupunguza kitu ile rasimu ya Tume.Hii siyo sahihi.

Kama Bunge la Katiba Halina mamlaka ya kuongeza, kupunguza, kuweka kitu basi Bunge Hilo kitakuwa ni Bunge lisilonameno ambalo Kamwe Watanzania Hatuwezi kuruhusu Kuwa na Bunge ambalo halina meno.

Kwa Mfano hiyo Rasimu ya Warioba ingekuwa imesahau Haki za watoto,wanawake. Bunge la Katiba lingebaini mapungufu hayo lisingekuwa na mamlaka ya kuweka Haki hizo?

Mbona kifungu cha 25(1) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012  iliyoandikwa kwa  lugha ya Kiingereza,  kinatoa mamlaka Kwa Bunge la Katiba Kutengeneza vifungu vipya  kuweka Masharti ya mapito ya Katiba inayopendekezwa.

Wakati Kifungu Cha 25 Cha Sheria hiyo ambayo imeandikwa Kwa lugha ya Kiswahili, Kinasema Bunge la Katiba linaweza ' kuboresha  na kurekesha... Katika kipungu hiki Kwenye Sheria hii iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili madaraka ya Bunge Hilo ni Kama yanapungua kwa Kusema ' linaweza kuboresha au kupunguza '. Wakati Sheria hiyo iliyoandikwa Kwa lugha ya Kiingereza inasema Bunge Hilo linaweza Kutengeneza vifungu Vya Sheria.

Sasa Kama huu ni mgogoro wa tafrisi ya Sheria hizo ambayo imeandikwa kwa lugha hizo mbili, Kifungu Cha 84 (3) Cha Tafsiri ya Sheria ya Mwaka 1996  Kinatamka wazi Kuwa panapotokea mgongano wa Tafsiri ya Sheria Moja iliyoandikwa kwa lugha mbili tofauti  basi Sheria iliyoandikwa kwa lugha ya kwanza ndiyo itayochukuwaliwa uzito na kutumiwa kumaliza Mzozo huo wa Tafsiri ya kisheria.

Ikumbukwe Kuwa Sheria ya Mabidiliko ya Katiba ya Tanzania iliandikwa kwa mara ya kwanza na kumpitishwa na Bunge Kwa lugha ya Kiingereza na Kisha Sheria hiyo ikajakutafsiriwa KWA lugha ya Kiswahili.Hivyo basi kwa mujibu wa Kifungu Cha 84(3) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria ya Mwaka 2012, ni Sheria iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza ndiyo itakayotumika.

Na wajumbe wote wa Bunge la Katiba walilidhia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012 iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza ndiyo itumike kuendeshea Bunge na Bunge Hilo likalidhia Kuwa Lina mamlaka ya Kutengeneza vifungu upya Vya Sheria Kama ilivyoelezwa Kwenye Kifungu Cha 25(1) Cha Sheria hiyo ya mabadiliko ya Katiba pindi Iinapoona kuna haja ya kufanya hivyo.

Leo hii baadhi ya wajumbe Hao wanavyose Bunge Hilo halina mamlaka ya kutunga vifungu vipya na kufanyia marekebisho rasmi hiyo ni wazi ni wanafki na wazandiki  Kwani wanapingana na maamuzi Yao ya awali waliyolodhiia ndani ya Bunge kuwa Bunge Hilo Lina mamlaka ya kutunga, kurekebisha.

UKAWA wameapa  kutorejea bungeni ambapo Bunge Hilo linaanza Agosti 5 Mwaka huu la Madai Kuwa wamechoshwa na lugha za kejeli,baadhi ya wajumbe kumtusi Jaji Warioba, mchakato wa Katiba mpya Tayari umeishachakachuliwa na wajumbe Toka CCM licha ya Makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa dini Kuwaasa ware je bungeni wakati ile majukumu Yao ya Kutengeneza Katiba Mpya ambayo wamekuwa wakidai kwa MUDa mrefu.

Ni kweli awamu ya kwanza ya Kikao Cha Bunge Maalum tulishuhudia upuuzi na uhuni wa Hali ya juu uliofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Hilo Hali iliyosabisha heshima ya Bunge Hilo kushuka na wananchi kukerwa na vitendo hivyo.Wajumbe wa Ukawa wao waliamua kususia Bunge Hilo kwa kile walichodai watolewa lugha chafu na baadhi ya wajumbe wenzao ambao wakidai ni wajumbe toka CCM na Mwenyekiti wa Bunge Hilo Hawachukulii Hatua yoyote.

 Kwa wale tuliokuwa tunalifuatilia Bunge la Katiba ni kweli tulishuhudia baadhi ya wabunge wa Ccm wakiwatolea lugha za kuudhi baadhi ya wajumbe ambao wamejitambulisha ni Ukawa na baadhi ya wanachama wa Ukawa nao tuliwashuhudia ndani ya Bunge nao walitumia lugha za kejeli dhidi ya wajumbe wenzao  Hali iliyosabisha kwa watu wenye akili timamu na wanaojiheshimu kuwaona wote Hao  ni wahuni na Hakuna mwenye afadhali na vitendo vyao vya kihuni vinadhalilisha  bunge letu.

Wakati vitendo hivyo Vya kifedhuli vikifanyika ndani ya Bunge, Bunge Hilo lilikuwa Halina Kanuni zinazoweza kuwabana wajumbe wanatoa lugha chafu na kuudhi wenzao, kumjadili mtu  badala ya kujadili rasimu, kuwabana wale wajumbe wanaosusia  Bunge hilo, na wajumbe wanaamishia nje ya bunge mjadala wa kutengeneza katiba.

Kwa Kuwa Hakuna na Kanuni hizo ndiyo mAana miongoni mwa wajumbe wakawa wanatumia mwanya huo kufanya ufedhuli huo Kwani walikuwa wanafahamu fika Hakuna Sheria wala Kanuni ya kuwabana.

Udhahifu huo uwe ni Changamoto kwa Bunge la Katiba kupitia Kamati yake ya Kanuni , itunge  Kanuni za Kuzuia ufedhuli huu usiiendelee Katika Kikao kijacho. Binafsi naitaji Katiba mpya itengenezwe kwa kufuata Taratibu zote na wanaoitengeneza wawe na nidhamu na wajiheshimu.

Binafsi nawashauri   UKAWA  warejee bungeni Na hoja Yao Yakutaka muundo wa serikali Tatu na wapigie kura hiyo katiba itakayopendekezwa na Bunge Hilo KWA Wingi na Hilo kundi la wajumbe toka CCM nao wapigie kula za ndiyo muundo wa serikali mbili na kwakuwa UKAWA  wameishatamba Kuwa wana theluthi mbili za wajumbe toka Zanzibar  basi hiyo hoja Yao waingie  nayo  ndani ya Bunge kwa Amani na wapigie kula hiyo Katiba inayopendekezwa na Bunge wanaweza wakashinda Kama kweli wanaowajumbe Wengi.
  
UKAWA kama dai lao la kwamba wananchi Wengi wanataka muundo wa serikali Tatu. Basi hiyo Katiba itakayopendekezwa na Bunge Maalum itakapopelekwa Kwa Hao wananchi ambao Ukawa wamedai wanataka muundo wa serikali Tatu , basi wananchi wanapiga kula nyingi za Ndio za kutaka muundo wa serikali Tatu.Tatizo linatoka wapi?

Hoja yangu kwa UKAWA je Leo hii wakiakikishiwa Kuwa lugha za matusi, kejeli hazitakuwepo tena bungeni ,wanakubali Kurejea bungeni kuendelea na mchakato wa Kutengeneza Katiba?
 
Mwisho , naomba ieleweke wazi Kuwa hapa nchini Kuna watu wanaheshimika sana lakini ilipotokea Mzozo huu wa UKAWA  wajivunjia heshima zao Kwa kutoa maoni Yao ambayo hayasaidii Kuleta maridhiano Bali kuongeza Chuki.Namalizia kwa Kusema yaliyo pita Si ndwele,tugange yajayo.

Tofauti za pande zote mbili za wajumbe wa Bunge Maalum zizikwe ,tufungue ukurasa mpya ,UKAWA rudi ni bungeni mkatimize majukumu yenu Kama mlivyoapa kwa mustakabali wa taifa letu Kwani Hao hao wanajifanya wanawaunga  mkono Leo hii  KWA uamuzi wenu wa Kugoma Kurejea bungeni ndiyo Kesho watakuwa Wakwanza Kuwachafua Kuwa milikuwa na Lengo baya la kukwamisha upatikAnaji wa Katiba mpya.

Mungu ibariki Tanzania
0716 774494 

No comments:

Post a Comment