WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, August 14, 2014

KIKWETE: SERIKALI HAINA MAMLAKA YA AMRI KUZUNGUMZIA URAIA PACHA.


IMG_9796
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya MkrishoKikwete akiingia ukumbini wakati wa kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.Nyuma yake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizend Pinda( mwenye koti la Bluu).Hassan Silayo-MAELEZO
IMG_9810(1)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Watanzania waishio Nje ya Nchi Bw.Emannuel Mwachulla akitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa mchangowake katika masuala ya kuwadhamini watanzania waishio Ughaibuni, wakati wakongamano la Watanzania waishio nje ya Nchi lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9842
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9895
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni na kusisitiza kuhusu wajibu wao wa kukumbuka nyumbani na kuendelea kuchangia katika masuala lauchumi na kijamii kwa ujumla kwa ajili ya maendeleo ya nchi

IMG_9921
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibunilililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.
Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo. 
IMG_9926
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya MrishoKikwete akiangalia tovuti ya Umoja wa Watanzania waishio nje ya baada yakuizindua tovuti hiyo leo jijini Dar es Salaam.
IMG_9929
Mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Leticia Nyerere (Kushoto) akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano laWatanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini
IMG_9934
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9940
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibunilililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………….
Na Joseph Ishengoma
MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema
hana mamlaka ya amri kuzungumzia uraia pacha kwasababu ni la katiba.
Rais Kikwete amesema hayo leo katika kongamano la kwanza la diaspora
lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam. Diaspora ni lugha
inayotumika kuwatambulisha Watanzania walioko nje ya nchi wanaojiendeleza
kwa njia mbalimbali ikiwemo elimu.
Kongamano hilo la siku mbili lenye lengo la kuelimishana, kubadilishana mawazo
na kujadili fursa za uwekezaji, linaudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 17 duniani.
“Serikali imelisikia suala la uraia pacha, lakini ni la kikatiba sio la Rais. Katiba
ndio sheria mama sisi hatuna mamlaka ya amri kulizungumzia.”
Kwa mujibu wa Rais, watanzania waliowengi uraia pacha hauwakeleketi, hivyo
diaspora wanaoishi nje ndio wanaostahili kulisukuma, lakini kwa sasa sauti
yao bado haijasikika sana, badala ya kulizungumzia kwa nguvu, wanatumia
muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani kwenye mitandao ya kijamii pindi
wanapopata nafasi.
“Sauti yenu haijasikika sana, badala yake mnatumia muda mwingi kuzungumzia
siasa za mitaani. Suala la uraia pacha liko mikononi mwa Bunge Maalum la
Katiba. Kama katiba haijasema nyinyi ni rais, sheria ikitungwa haiwezi kuwapa
uraia,” amesema.
Kwa mujibu wa Rais, rasmu ya Katiba iliyopo inazungumzia hadhi ya Watanzania
walioko nje sio uraia. “Mnachoweza kufanya ni kushawishi wabunge wa Bunge
Maalum la Katiba kukubali uraia pacha kuwa ndani ya katiba na hili sio jambo
haramu, zungumzeni nao serikali haina tatizo nalo iwapo Katiba itawatambua.”
Pamoja na uraia pacha, Rais amewaomba wanadiaspora kuzingatia uwekezaji
ndani ya nchi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kutafuta masoko ya bidhaa ya
bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuunda umoja utakaowaunganisha na kutumia
teknolojia na maalifa wanayopata nje kuendeleza taifa lao.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni, “Nyumbani ni Nyumbani.”
Awali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Mizengo kayanza Pinda
ametaka mkutano huo kusaidia kukata kiu ya Watanzania kupata majibu ya mambo
ambayo wamekuwa wakiulizia pindi wanapokutana na viongozi mbalimbali wan
chi nje ya Tanzania.
PICHA NA IKULU
source: matukio na vijana

No comments:

Post a Comment